Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

Biden aapa kutetea Ufilipino iwapo litatokea 'shambulio' katika Bahari ya China Kusini

Katika onyo lililolenga Beijing, Joe Biden aliahidi siku ya Alhamisi kuilinda Ufilipino katika tukio la "mashambulizi" katika Bahari ya Kusini ya China, wakati wa mkutano wa kilele wa kipekee na viongozi wa Japan na Ufilipino.

Rais Joe Biden, katikati, akizungumza pamoja na Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr., kushoto, na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida kabla ya mkutano wa pande tatu katika Ukumbi wa Mashariki ya Ikulu ya Marekani mjini Washington, Alhamisi, Aprili 11, 2024.
Rais Joe Biden, katikati, akizungumza pamoja na Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr., kushoto, na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida kabla ya mkutano wa pande tatu katika Ukumbi wa Mashariki ya Ikulu ya Marekani mjini Washington, Alhamisi, Aprili 11, 2024. AP - Mark Schiefelbein
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani alitangaza kwamba "shambulio lolote dhidi ya ndege, meli au vikosi vya jeshi vya Ufilipino katika Bahari ya Kusini ya China vitaanzisha utekelezaji wa mkataba wa ulinzi wa pande zote" ambao unazihusisha Washington na Manila.

Saa chache baadaye, viongozi hao watatu walionyesha katika taarifa ya pamoja "wasiwasi wao mkubwa juu ya tabia hatari na ya uchokozi ya Jamhuri ya Watu wa China katika Bahari ya Kusini ya China", wakisema hasa "kuhangaishwa na uvamizi wa kijeshi wa maeneo yaliyopatikana na kwa madai haramu ya baharini” katika eneo hili la kimkakati.

Rais Joe Biden alimpokea Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos na Waziri Mkuu Fumio Kishida katika Ikulu ya White House wakati wa mkutano wa kilele wa nchi tatu ambao haujawahi kushuhudiwa, dhidi ya matukio kadhaa ya mfululizo yaliyohusisha China katika eneo hili la baharini.

"Kujitolea kwa Marekani kwa usalama wa Japani na Ufilipino ni lazima," alisema rais Biden, mwenye umri wa miaka 81.

Alizungumza juu ya lengo la pamoja la eneo "huru, la wazi, lenye mafanikio na salama" la Asia-Pasifiki, usemi wa kawaida unaotumiwa na Marekani kurejelea miradi inayodhaniwa, kinyume chake, hatari na fujo na China.

Mamlaka ya China tayari imejibu kwa ukali tangazo hilo, lililotolewa siku ya Jumatano, la kuongezeka kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Marekani na Japan.

"Marekani na Japan, bila kujali wasiwasi mkubwa wa China, zimechafua na kushambulia China juu ya maswala ya Taiwan na baharini," Mao Ning, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, alisema katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari.

Rais wa Marekani alimpokea Fumio Kishida Jumatano kwa ziara ya kifahari, utangulizi wa mkutano huu wa pande tatu na Ferdinand Marcos, mtoto mwene jina la dikteta wa zamani wa Ufilipino, aliyeingia madarakani mwezi Juni 2022.

- "Changamoto kubwa ya kimkakati" -

Mkuu wa nchi ya Ufilipino alikaribisha mkutano wa "kihistoria", kwa maneno mafupi mbele ya waandishi wa habari. "Mkutano wa leo unatupa fursa ya kufafanua siku zijazo tunazotaka na njia za kuifanikisha kwa pamoja," aliongeza.

Hatua za kijeshi za China "zinawakilisha changamoto isiyo na kifani, na changamoto kubwa zaidi ya kimkakati sio tu kwa amani na usalama wa Japani lakini kwa amani na usalama wa jumuiya nzima ya kimataifa," Waziri Mkuu wa Japan alisema, mapema Alhamisi, mbele ya Baraza la Congress la Marekani.

Katika miezi ya hivi karibuni, mivutano kati ya China na Ufilipino - ambayo inazidi kudai madai yao ya eneo - imefikia viwango ambavyo havijaonekana kwa miaka kadhaa.

Chanzo: mfululizo wa matukio tangu mwisho wa mwaka 2023 karibu na miamba inayozozaniwa katika Bahari ya China Kusini.

Mwezi uliopita, meli za China na Ufilipino ziligongana mara mbili, matukio yaliyotokea karibu na Atoll Second Thomas, eneo ambalo China inaliita Ren'ai .

Katika muktadha huu, Joe Biden alitangaza kwamba Marekani, Ufilipino na Japan "zitaimarisha uhusiano wao katika masuala ya usalama wa baharini".

Pia aliahidi ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia, hasa kuendeleza miradi mikubwa ya miundombinu nchini Ufilipino.

Joe Biden amejitolea kuunganisha mtandao mkali wa ushirikiano katika Asia-Pasifiki ili kukabiliana na malengo ya kimkakati ya China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.