Pata taarifa kuu

Papa Francis hivi karibuni kuzuru nchi nne za Asia na Oceania

Vatican imetangaza leo Ijumaa, Aprili 12, kwamba kiongozi wa kanisa Katoliki anatarajia kufanya ziara mpya ya kitume katika bara la Asia na Oceania. Papa Francis anatarajiwa kuzuru nchini Indonesia, Papua New Guinea, Timor Mashariki na Singapore kuanzia Septemba 2 hadi 13. Safari ya kilomita 30,000 imethibitishwa licha ya afya dhaifu ya kiogozi wa kanisa Katoliki duniani.

Vatican imetangaza Ijumaa hii, Aprili 12, ziara mpya ya kitume ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki. Papa Francis anatarajiwa kuzuru Indonesia, Papua New Guinea, Timor Mashariki na Singapore kuanzia Septemba 2 hadi 13.
Vatican imetangaza Ijumaa hii, Aprili 12, ziara mpya ya kitume ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki. Papa Francis anatarajiwa kuzuru Indonesia, Papua New Guinea, Timor Mashariki na Singapore kuanzia Septemba 2 hadi 13. AFP - MIGUEL RIOPA
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Korea Kusini, Ufilipino na Japan, Papa Francis ataongeza ziara mpya huko Asia kwenye orodha ya safari zake za kitume, anaripoti mwandishi wetu huko Roma, Éric Sénanque.

Nchi zilizo na utofauti mkubwa sana ambapo jamii za Kikatoliki ni zimetawanyika, wakati mwingine wachache sana kama vile Indonesia ambako ni chini ya 3%. Indonesia, ambayo ni ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani, imesema katika taarifa yake siku ya Ijumaa kwamba ziara hii ya Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani ni "ya umuhimu mkubwa (...) sio tu kwa Wakatoliki, bali pia kwa jumuiya zote za kidini".

Zaidi ya Wakristo milioni tisa - karibu wakazi wote - wanaishi Papua New Guinea. Dini ya Kiprotestanti, hata hivyo, ndiyo iliyo na waumini wengi katika nchi hii ambayo pia imesalia kuwa na mila za animist (kuabudu vitu. Hakuna papa aliyezuru nchi hiyo tangu John Paul II mnamo 1995.

Ziara ambayo mada zake kali zinapaswa kuwa mazungumzo ya kidini, maridhiano kama vile Timor Mashariki au hata ikolojia nchini Papua New Guinea. 

Mwezi wa Januari mwaka huu, Papa Francis alisisitiza nia yake ya kutembelea Asia kwa mara nyingine tena. Baadhi ya hatua hizi, kama vile Indonesia, zilikuwa kwenye ajenda mnamo mwaka 2020, lakini zilifutwa kwa sababu ya janga la UVIKO. Safari hii ya siku kumi na moja katika nchi nne itakuwa ndefu zaidi kati ya papa kutoka Argentina, mwenye umri wa miaka 87 baada ya matatizo yake mengi ya kiafya katika miezi ya hivi karibuni. Mwezi wa Desemba mwaka uliyopita, Papa Francis alilazimika kufuta ziara yake huko Dubai katika dakika ya mwisho kwa mkutano wa tabianchi wa Umoja wa Mataifa.

Tangazo hili linakuja baada ya wasiwasi juu ya afya ya Papa Francis wakati wa likizo ya Pasaka: akionekana amechoka, alikuwa amefuta ushiriki wake katika hafla kuu ya Wiki Takatifu na kukabidhi usomaji wa hotuba zake, akitoa mfano wa ugonjwa wa mkamba. Jorge Bergoglio, ambaye amekuwa akitumia kiti cha magurudumu kwa miaka miwili, amepata matatizo ya kiafya katika miaka ya hivi karibuni, hasa magoti, nyonga na utumbo mpana, na ana matatizo ya kupumua.

Kwa zaidi ya saa 30 za mwendo wa safari, tofauti ya saa nane, mfululizo wa mikutano na misa, safari hii itawakilisha changamoto kubwa sana ya kimwili kwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.