Pata taarifa kuu

China: Rais Xi Jinping ampokea mkuu wa zamani wa Taiwan Ma Ying-jeou

Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa zamani wa Taiwan kukaribishwa kwa njia hii mjini Beijing tangu mwaka 1949. Ma Ying-jeou alipokelewa siku ya Jumatano kwa heshima kamili na Xi Jinping katika Ukumbi Mkuu wa Watu, Tiananmen Square. Hafla hiyo, iliyoangaziwa sana na vyombo vya habari vya serikali ya China, inalenga kukuza umoja.

Katika picha hii iliyotolewa na Shirika la Habari la Xinhua, Rais wa China Xi Jinping, kulia, akipeana mkono na rais wa zamani wa Taiwan Ma Ying-jeou wakati wa mkutano wao huko Beijing Jumatano, Aprili 10, 2024.
Katika picha hii iliyotolewa na Shirika la Habari la Xinhua, Rais wa China Xi Jinping, kulia, akipeana mkono na rais wa zamani wa Taiwan Ma Ying-jeou wakati wa mkutano wao huko Beijing Jumatano, Aprili 10, 2024. © Ju Peng/Xinhua via AP
Matangazo ya kibiashara

Kwa hafla hiyo, ambayo imebadili taswira ya viongozi wawili wazee waliozungukwa na kundi la wanafunzi kutoka ujumbe wa Taiwan wakikaribisha makubaliano, tofauti na mvutano wa miezi ya hivi karibuni kati ya Taipei na Beijing.

Picha ya wawili hawa ilirushwa na kuwa gumzo siku ya Jumatano nchini Uchina, mamlaka ya kikomunisti hapa ikilipiza kisasi cha vyombo vya habari juu ya ushindi mkubwa wa Chama cha Kidemokrasia cha Maendeleo wakati wa uchaguzi wa urais wa Taiwan mwezi Januari maka huu.

"Familia moja"

“Watu wa pande zote za Mlango-Bahari wa Taiwan wote ni Wachina. "Hakuna mzozo ambao hauwezi kutatuliwa, hakuna suala ambalo haliwezi kujadiliwa, na hakuna nguvu inayoweza kututenganisha," Xi Jinping amesema, akimaanisha "familia moja" inayopinga uingiliaji wa nje.

"Tofauti kati ya mifumo hiyo haiwezi kubadilisha ukweli kwamba pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan ni za nchi moja na taifa moja," ameongeza rais wa China, akipendelea kumuinua kwa jina la "Bwana" Ma Ying-jeo kwa mgeni wake, ili kuepuka kutaja hadhi yake kama rais wa zamani - kati ya mwaka 2008 na 2016 - ikifahamika kwamba Beijing na Taipei hazitambuani rasmi.

Ma Ying-jeou amejibu kwamba vita vipya kati ya pande hizo mbili vitakuwa mzigo usiobebeka kwa taifa la China, kwani meli na ndege za China zimeongeza ziara zao karibu na kisiwa hicho katika wiki za hivi karibuni. China inachukulia Taiwan kama moja ya majimbo yake yanayotakiwa kuunganishwa tena.

"Ziara ya Amani"

Bila kujumuishwa katika kampeni mbaya ya Kuomintang (KMT), chama cha upinzani cha Nationalist nchini Taiwan, Ma Ying-jeou, 73, alianza ziara ya China bara mnamo Aprili 1 ambayo anaielezea kama "ziara ya amani."

Yule ambaye tayari alikutana na Xi Jinping nchini Singapore mwishoni mwa muhula wake wa kwanza mwaka 2015, anatetea mstari wa maridhiano na Beijing ambao unatofautiana na matakwa ya wapiga kura wengi nchini Taiwan. "Wazalendo wa pande zote mbili wameunda familia moja kila wakati, na wanapaswa kutembeleana mara kwa mara na kuwa karibu zaidi na wenye upendo," rais wa China, wakati China bara bado haijafungua tena uwezekano wa kusafiri kwa mtu mmoja mmoja nchini Taiwan.

Ziara hii rasmi inajiri wakati Joe Biden akimpokea Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida mjini Washington, na Lai Ching-te wa Chama cha Maendeleo cha Kidemokrasia cha Taiwan atachukua madaraka kama rais wa Taiwan Mei 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.