Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-JAPAN-KOREA KUSINI-USALAMA

Seoul na Tokyo wakaribisha onyo la Trump dhidi ya Pyongyang

Vitisho vya Donald Trump vya "kuisambaratisha Korea Kaskazinia" vilivyotolewa na rais wa Marekani Donald Trump kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa vitaiwezesha haraka Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa nyuklia, Korea Kusini imesema Jumatano hii.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in akimsabahi Joseph Dunford, Mkuu wa Majeshi ya Marekani, tarehe 14 Agosti 2017 Seoul.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in akimsabahi Joseph Dunford, Mkuu wa Majeshi ya Marekani, tarehe 14 Agosti 2017 Seoul. Bae Jae-man/Yonhap via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne, katika hotuba yake ya kwanza kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, rais wa Marekani alitoa onyo kali dhidi ya Korea ya Kaskazini, ambapo aliitisha "kuisambaratisha kabisa" ikiwa itahitajika kwa kuilinda Marekani. Marekani.

"Tunaona hotuba hii kama mfano wa msimamo thabiti na sahihi juu ya masuala muhimu ya kulinda amani na usalama ambayo jumuiya ya kimataifa na Umoja wa Mataifa wanakabiliana nayo," ofisi ya rais wa Korea Kusini imebaini katika taarifa yake.

"Hii inaonyesha wazi umuhimu wa serikali ya Marekani kwa mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini, ambapo rais ametumia muda mrefu kwa swala hilo," Seoul imeongeza.

"Korea Kaskazini kupitia vikwazo na shinikizo la kutosha linapaswa kutambua kwamba kuachana na mpango wa nyukilia ndiyo njia pekee ya baadaye."

Jae-in, ambaye aliteuliwa mwezi Mei juu ya kufufua upya mazungumzo na Korea Kaskazini, alikabiliwa na ongezeko la majaribio ya makombora ya masafa marefu ya Pyongyang pamoja na jaribio la mwisho la nyuklia la Septemba 3.

Rais wa Korea Kusini, ambaye alibaini kuwa muda huu si wa majadiliano, anapanga kukutana na Donald Trump mjini New York Jumatano hii asubuhi, saa za Pwani ya Mashariki, washauri wake wamesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.