Pata taarifa kuu
UN-KOREA KAZKAZINI-USALAMA

Guterres aonya dhidi ya hatari ya vita na Korea Kaskazini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameomba Jumanne hii kuewepo na "ulimwengu bila silaha za nyuklia", akionya dhidi ya hatari ya vita na Korea Kaskazini.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres tarehe 19 Septemba 2017.  New York.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres tarehe 19 Septemba 2017. New York. AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake ya kwanza kwa marais na viongozi wa serikali 130 wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kwamba suluhu na Pyongyang "inapaswa kuwa ya kisiasa" na kwamba kuna ulazima wa kuepuka "vita".

"Natoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuendeleza umoja" katika mgogoro na nchi hii, ameongeza Antonio Guterres, akifunguliwa rasmi mjini New York Mkutano Mkuu wa mwaka wa Umoja wa Mataifa ambao unazikutanisha mataifa 193. "Umoja pekee ndio utawezesha kuachana na nyuklia ya rasi ya Korea na kuanzisha uwezekano wa ushirikiano wa kidiplomasia ili kutatua mgogoro huo".

Wakati ambapo Korea Kaskazini ikiendelea na mpango wake wa nyuklia na majaribio ya kufyatua makombora ya masafa marefu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza kwa miezi kadhaa maazimio yanayoweka vikwazo vikali vya kiuchumi Dhidi ya Pyonyang.

Rais wa Marekani Donald Trump mpaka sasa hajaonyesha kama kweli anaamini kabisa mchakato wa vikwazo unaweza kuileta KoreaKaskazini kwenye meza ya mazungumzo. Mara kadhaa alitumia kauli ya uwezekano wa kutumia nguvu ili kuishinikiza Pyongyang kuja kwenye meza ya mazungumzo na kuachana na mpango wake huo wa nyuklia.

Siku ya Jumatano, mataifa ya kwanza yataanza kusaini kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mkataba unaopiga marufuku silaha za nyuklia. Nchi zaidi ya 120 zimekubali mkataba huu mapema katika majira ya joto ambao unalenga kuimarisha maamuzi dhidi ya silaha zinazoenea duniani kupitia makundi mbalimbali. Njia hii imekataliwa na nchi zinazotengeneza silaha za nyuklia, ikiwa ni pamoja na wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.