Korea Kaskazini yataka usawa wa kijeshi na Marekani
Korea Kaskazini jana Jumamosi imesema kuwahaitashushwa chini kwa lolote bali inataka usawa wa kijeshi na hasimu wake Marekani kwa ukamilifu wa silaha za nyuklia, hatua ambayo imelazimisha baraza la Usalama la umoja wa Mataifa kuwa na mazungumzo mapya kuhusu mgogoro huo
Imechapishwa:
Kim Jong-Un alifanikiwa siku ya Ijumaa alifanikiwa kurusha kombora la Hwasong-12 la masafa ya kati juu ya Japan, akijibu vikwazo vya karibuni vya Umoja wa Mataifa kuhusu jaribio lake la sita la nyuklia.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakuwa na mkutano siku ya Alhamisi mkutano ambao utajikita kutafuta namna nzuri ya kutekeleza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini ili kuondoa kitisho cha kuenea kwa silaha za maanagamizi duniani.
Marekani imeitisha kikao hicho ambacho kitafanyika wakati wa mkutano Mkuu wa kila mwaka wa viongozi wa dunia kwenye Umoja wa Mataifa.