Pata taarifa kuu
DRC-ICC-UHALIFU-USALAMA

Bensouda aitaka DRC kuchunguza vitendo vya ukiukaji wa haki za binandamu

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya Kimataifa ya ICC Fatou Bensouda amekamilisha ziara yake nchini DRC ambako amekutana na watu mbali mbali akiwemo rais Joseph Kabila.

Fatou Bensouda, Mwendesha Mashitaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC.
Fatou Bensouda, Mwendesha Mashitaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC. ICC-CPI
Matangazo ya kibiashara

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Gambian Fatou Bensouda, alikutana na Joseph Kabila huko Kinshasa. Hasa, walijadili vurugu katika DRC, hali ya mahakama ya kitaifa na ushirikiano kati ya Ofisi ya ICC na DRC.

Bensouda alikutana na Rais Joseph kabila, serikali, bazara la maaskofu, upinzani, wanasheria na mashirika ya kiraia. Bi Fatou Bensouda alikuja kuulizia hali ya haki za binadamu. Kwa mujibu wa Fatou Bensouda, serikali ina jukumu la msingi la kuanzisha kesi za kisheria dhidi ya wahalifu wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini DRC kwa lengo la kukomesha kutokujali na kurejesha hali ya haki na amani nchini.

“Nimeelezea wasiwasi wangu kuhusu hali mbaya na matukio ya vurugu yalioriipotiwa hasa Kinshasa, Beni, mikoa ya Kasai na maeneo mengine ya DRC. Tumeamua kuimarisha wezo wetu wa kuzuia unyanyasaji na kuwashtaki wale wanaosababisha uovu uliofanywa nchini DRC, katika hali ya ushirikiano kulingana na Sheria ya Roma ilio sainiwa na DRC, “ amesema Bi Bensouda

Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Kidemocratia ya Congo, Flory Kabange Numbi, alimhakikishia Mwendesha Mashitaka wa ICC uamuzi wa mamlaka za Kinshasa kuchunguza kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu na kufungua mashitaki dhidi ya wahalifu hao.

Baada ya mkutano wake na wanahabari, Fatou Bensouda alikutana na upinzani wa mkoa wa Kivu Kaskazini waliomtolea malalamiko yao wakibani kwamba raia wengi waliuawa katika maeneo tofauti ya mko hup, hasa katika wilaya ya Beni.

Mnamo Machi 2016, afisa mkuu wa ICC Margot Tedesco, alisema kuwa Mahakama ya ICC tayari imepokea taarifa kuhusu mauaji huko Beni, Kivu kaskazini . Ameonyesha kuwa ofisi yake imeanza kufanyia kazi taarifa hiyo "bila upendeleo na kujitegemea".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.