Pata taarifa kuu
HAKI-DEMOKRASIA

Katiba mpya ya Togo: Upinzani wawasilisha malalamiko yake ECOWAS

Vyama 13 vya kisiasa na mashirika ya kiraia nchini Togo yamewasilisha malalamiko yao mbele ya Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kutaka Katiba mpya ya nchi hiyo iondolewe, kwa mujibu wa nyaraka ambazo shirika la habari la AFP limepata kopi.

Mabango ya wagombea kwenye nafasi ya ubunge, Aprili 24, 2024 nchini Togo.
Mabango ya wagombea kwenye nafasi ya ubunge, Aprili 24, 2024 nchini Togo. © DODO ADOGLI / AFP
Matangazo ya kibiashara

ECOWAS imelithibitishia shirika la habari la AFP kwamba imepokea malalamiko ya upinzani na mashirika ya kiraia yaliyowasilishwa Aprili 18, siku moja baada ya kupitishwa kwa hatu ya mwisho kwa Katiba mpya na wabunge nchini Togo, na wakati uchaguzi wa wabunge na mikoa umepangwa kufanyika Aprili 29.

Miongoni mwa vyama vya siasa na mashirika ya kiraia yaliyowasilisha malalamiko hayo ni vyama kadhaa vya upinzani, vikiwemo National Alliance for Change (ANC), Alliance of Democrats for Integral Development (ADDI) au Democratic Forces for the Republic (FDR) na mashirika kama vile Ligue Togo for Human Rights au Chama cha waathiriwa wa Mateso nchini Togo (Asvitto). Wanaiomba Mahakama ya Haki ya ECOWAS "kushtumu Jamhuri ya Togo" kwa kuwa imebadilisha Katiba yake, na "kuondoa kabisa sheria ya mabadiliko ya katiba".

Upinzani unahofia kwamba katiba hiyo mapya itaruhusu kurefushwa kwa muhula wa mkuu wa nchi Rais Faure Gnassingbé, aliye madarakani tangu mwaka 2005 baada ya babake mwenyewe ambaye alihudumu kwa karibu miaka 38. Chini ya masharti ya Katiba mpya, ambayo yatabadilisha nchi kutoka utawala wa rais hadi utawala wa bunge, rais atachaguliwa kwa muhula wa miaka minne, ambao unaweza kurejeshwa upya mara moja, na wabunge na sio tena na wananchi.

Madaraka sasa yatakuwa mikononi mwa aina ya Waziri Mkuu ambaye lazima awe "kiongozi wa chama kilicho wengi" katika Bunge la taifa. Kiongozi wa chama kilichoshinda katika uchaguzi wa Aprili 29 atateuliwa kwa nafasi hii mpya. Rais wa chama kilicho wengi kwa sasa katika Bunge hilo, Union for the Republic (UNIR), si mwingine ila Faure Gnassingbé.

Katika ombi lao kwa ECOWAS, wanaona kuwa mageuzi ya katiba "yalifanywa bila kuwepo kwa mjadala wa awali wa umma na makubaliano ya kisiasa", ambayo yanadhoofisha "demokrasia na utawala bora". Wanadai kuwa "wamekuwa waathiriwa wa ukiukwaji wa haki zao, kitendo kinachofanywa na serikali ya Togo", ambayo ilipiga marufuku maandamano yaliyopangwa na upinzani.

Siku ya Jumatano, Mahakama ya Kikatiba ya Togo ilikataa ombi la vyama viwili vya upinzani (NET na PDP) vilivyoiomba itoe uamuzi kuhusu Katiba mpya. Mwanahistoria wa Togo Michel Goeh-Akue, aliye karibu na upinzani, ameliambia shirika la habarila AFP kwamba upinzani haujidanganyi kwa kutumia njia hii kwa ECOWAS, ambayo kulingana naye imekuwa "ganda tupu na taasisi inayotumiwa kupita kiasi.

Mnamo mwezi Desemba, Mahakama ya Haki ya ECOWAS, iliyopokea malalamiko kutoka kwa mawakili wa Mohamed Bazoum, rais wa Niger aliyeondolewa madarakani na mapinduzi ya kijeshi ya Julai 2023, iliamuru kuachiliwa kwa mkuu huyo wa zamani wa serikali ya Niger pamoja na kurejea madarakani. Uamuzi ambao haujatekelezwa hadi sasa, jeshi lililo madarakani huko Niamey bado linapinga kuachiliwa kwa Mohamed Bazoum.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.