Pata taarifa kuu

Uingereza yatakiwa kubatilisha mpango wake wa kutuma waomba hifadhi Rwanda

Tume ya kutetea haki za binadamu barani Ulaya, imetoa wito kwa Uingereza kutupilia mbali mpango wake wenye utata wa kuwatuma waomba hifadhi nchini Rwanda, wito unaokuja baada ya bunge jijini London kupitisha mswada huo.

Mapango huo tangu kupendekezwa umekuwa ukikabiliwa na changamoto kadhaa za kisheria, watetezi wa haki za binadamu wakiupinga.
Mapango huo tangu kupendekezwa umekuwa ukikabiliwa na changamoto kadhaa za kisheria, watetezi wa haki za binadamu wakiupinga. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kamishena wa tume hiyo barani Ulaya Michael O'Flaherty, mpango huo kati ya serikali ya Kigali na ile ya Uingereza, unaibua maswali mengi kuhusu haki za waomba hifadhi na sheria kwa ujumla.

Bunge nchini Uingereza siku ya Jumatatu lilipitisha mswada unaoruhusu kutumwa kwa waomba hifadhi nchini Rwanda wakati wakisubiri uamuzi kuhusu maombi lao.

Soma piaBunge la Uingereza lapitisha mswada wa kuwafukuza wahamiaji na kuwapeleka nchini Rwanda

Aidha kamishena huyo ameelezea wasiwasi wake  kwamba mswada huo unawezesha utekelezaji wa sera ya kuwaondoa watu kwenda Rwanda bila tathmini ya awali ya madai yao ya kuomba hifadhi na mamlaka ya Uingereza.

O'Flaherty pia alionya kuwa mswada huo unazuia kwa kiasi kikubwa mahakama za Uingereza kuangazia kikamilifu na kwa uhuru maswala yanayowasilishwa mahakamani.

Mpango huo ambao umekashifiwa na wataalam wa masuala ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa na makundi yanayotetea haki za waomba hifadhi, umekabiliwa na changamoto za kisheria tangu ulipopendekezwa mwaka wa 2022.

Serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak imekuwa ikikabiliwa na shinikizo la kukabiliana na idadi kubwa ya waomba hifadhi wanaoingia nchini humo wakitokea kaskazini mwa Ufaransa kwa kutumia boti ndogo.

Umoja wa Mataifa pia umetoa wito kwa Uingereza kuangazia upya mpango huo ikisema kuwa ni tishio kwa utawala wa sheria.

Uingereza inalenga kupunguza idadi ya waomba hifadhi wanaowasili nchini humo kwa wingi wakitokea kaskazini mwa Ufaransa kwa kutumia boti ndogo.
Uingereza inalenga kupunguza idadi ya waomba hifadhi wanaowasili nchini humo kwa wingi wakitokea kaskazini mwa Ufaransa kwa kutumia boti ndogo. © Daniel Leal / AFP

Tayari serikali ya Rwanda kupitia msemaji wake Yolande Makolo, imeeleza kufuraishwa na hatua ya bunge nchini Uingereza kupitisha muswada wenye utata wa kuwatuma waomba hifadhi jijini Kigali.

Msemaji huyo ameongeza kuwa serikali ya Kigali iko tayari kuwakaribisha waomba hifadhi watakaohamishwa nchini Rwanda.

Hillary Ingati RFI-Kiswahili/AFP

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.