Pata taarifa kuu
ICC-DRC-WAASI-RUFAA

Germain Katanga na Jean-Pierre Bemba wapoteza rufaa

Majaji wa rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC, wamesisitiza kuwa aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini DRC Germain Katanga, alipe fidia ya Dola Milioni 1 kwa waathiriwa wa mateso yaliyotekelezwa na waasi wake katika mkoa wa Ituri mwaka 2003.

Germain Katanga kiongozi wa zamani wa waasi nchini DRC
Germain Katanga kiongozi wa zamani wa waasi nchini DRC www.icc-cpi.int
Matangazo ya kibiashara

Katanga aliyehukumiwa jela miaka 12 na kutozwa faini hiyo ambayo aliamua kukata rufaa akisema hana uwezo wa kulipa fedha hizo.

Hata hivyo, Majaji wametofautiana na Katanga na kumtaka kulipa fedha hizo wakisema hana sababu ya kuepuka hilo.

Waathiriwa 297 waliotambuliwa kuteswa na waasi hao hasa kubakwa kwa wanawake na wasichana katika kijiji cha Bogoro, watalipwa Dola 250 kila mmoja.

Wakati uo huo, Mahakama hiyoΒ  imetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa Makamu wa rais Jean-PierreΒ Bemba aliyepatikana na kosa la kuwahonga mashahidi 14 kusema uongo ili kumtetea wakati kesi yake ikiendelea.

Bemba amefungwa mwaka mmoja zaidi na kutozwa faini ya ya Euro 300,000 kwa kosa hilo, ukiachilia mbali kifungo cha miaka 18 jela alichohukimiwa mwaka 2016 baada ya kuongoza vikosi vyake vya MLCΒ  kutekeleza uhalifu wa kivita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.