Pata taarifa kuu

Marekani yatangaza kuanza kwa majadiliano juu ya kuondoka kwa wanajeshi wake kutoka Niger

Marekani inatangaza mazungumzo kuanzia Alhamisi, Aprili 25 mjini Niamey na wawakilishi wa utawala wa kijeshi kwa nia ya kuwaondoa kwa mpangilio na kuwajibika wanajeshi wa Marekani nchini Niger.

Raia wa Niger na maafisa wa jeshi wanakusanyika barabarani kuandamana dhidi ya uwepo wa jeshi la Marekani, huko Niamey, Niger, Aprili 13, 2024.
Raia wa Niger na maafisa wa jeshi wanakusanyika barabarani kuandamana dhidi ya uwepo wa jeshi la Marekani, huko Niamey, Niger, Aprili 13, 2024. REUTERS - Mahamadou Hamidou
Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Marekani nchini Niger, Kathleen FitzGibbon, pamoja na Meja Jenerali Ken Ekman, mkurugenzi wa mikakati, ushirikiano na programu wa Kamandi ya Marekani, wanakutana Alhamisi hii huko Niamey na wawakilishi wa utawala wa kijeshi kuanza majadiliano juu ya zoezi hili , inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa msemaji wa wizara ya Ulinzi ya Marekani.

Kuendeleza juhudi za ushirikiano

Mazungumzo haya yanafuatia mazungumzo yanayoendelea tangu Julai 2023, ambapo Marekani haikuweza kufikia makubaliano na utawala wa kijeshi ili kuendeleza ushirikiano wake wa usalama. Hata hivyo, Marekani inasema "inajivunia kujitolea kwa pamoja kwa majeshi ya Marekani na Niger, ambayo yamechangia ipasavyo katika utulivu nchini na kanda hiyo."

Kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani kutafanywa kwa utaratibu na uwajibikaji, na serikali ya Marekani inasema iko wazi kudumisha uhusiano wenye nguvu baina ya nchi mbili na Niger, inasema Washington.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa maafisa wa kijeshi wa Marekani "watafanya mikutano ya ufuatiliaji huko Niamey wakati katika wiki ya Aprili 29 ili kuratibu na kuhakikisha mchakato wa uwazi wa kuondokakwa kikosi hiki kwa kuheshimiana. Bw. Anderson ni afisa wa maendeleo ya pamoja ndani katika makao makuu ya majeshi ya Marekani."

Hata hivyo, Naibu Waziriwa Ulinzi Kurt M. Campbell atazuru Niamey "katika miezi ijayo ili kujadili kuendelea kwa ushirikiano katika nyanja zenye maslahi ya pamoja." Marekani inasema kwa hakika imesalia kujitolea kuwa na uhusiano thabiti na Niger.

Washington "inathibitisha uungaji mkono wake kwa raia wa Niger katika mapambano yao dhidi ya ugaidi, maendeleo yao ya kiuchumi na mpito wao kuelekea utawala wa kidemokrasia."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.