Pata taarifa kuu

Sudan: UAE yakanusha kwa barua kwa Umoja wa Mataifa kuunga mkono RSF

Takriban mwezi mmoja baada ya shutuma zilizotolewa mwishoni mwa mwezi Machi na mwakilishi wa kudumu wa Sudan, hatimaye Falme za Kiarabu zimejibu. Katika barua iliyotumwa siku ya Jumatatu Aprili 22 kwa Baraza la Usalama, ujumbe wa Imarati kwa Umoja wa Mataifa unakanusha msaada wowote kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (FSR) vya Jenerali "Hemedti" na umekasirishwa.

Mamlaka ya Sudan ilshutumu Abu Dhabi kwa kuunga mkono RSF Hapa, Jenerali Mohamed "Hemedti" Hamdane Daglo, katikati, anatoa rambirambi zake kwa Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Falme za Kiarabu na Mtawala wa Abu Dhabi, baada ya kifo cha Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan,  hayati rais wa Falme za Kiarabu, huko Abu Dhabi, Falme za Kiarabu, Jumapili, Mei 15, 2022.
Mamlaka ya Sudan ilshutumu Abu Dhabi kwa kuunga mkono RSF Hapa, Jenerali Mohamed "Hemedti" Hamdane Daglo, katikati, anatoa rambirambi zake kwa Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Falme za Kiarabu na Mtawala wa Abu Dhabi, baada ya kifo cha Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan, hayati rais wa Falme za Kiarabu, huko Abu Dhabi, Falme za Kiarabu, Jumapili, Mei 15, 2022. © Abdulla Al Neyadi/Ministère des affaires présidentielles via AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix

Kutokana na shutuma hizo, mwakilishi wa Khartoum alilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuichukulia vikwazo Imarati, hatua ambayo iliikasirisha Abu Dhabi.

"Madai yasiyo na msingi": hivi ndivyo ujumbe wa Falme za Kiarabu kwenye Umoja wa Mataifa znavyoelezea shutuma za Sudan. zinaona tu kama "upotovu" kuwafanya watu kusahau "migogoro na hali ya kibinadamu" nchini Sudan.

Mnamo Machi 30, mwakilishi wa kudumu wa Sudan alituma barua ya kina kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa: malalamiko ya kurasa 78 - "ushahidi na picha zinazounga mkono", kulingana na wanadiplomasia wa Sudan - kuhalalisha vikwazo dhidi ya Falme za Kiarabu. Inahusu misaada iliyotolewa kwa FSR ya Jenerali Mohamed "Hemedti" Hamdane Daglo, katika vita dhidi ya jeshi la serikali. Pia kuna mazungumzo ya usambazaji wa silaha na mamluki, wote walivuka mpaka wa Chad, kwa ushirikiano wa Ndjamena.

Madai haya si mapya. Viongozi wa Sudan pia wamekuwa wakilalamika kwa wiki kadhaa kwamba mamlaka ya Port Sudan wamekuwa wakiomba misaada ya kibinadamu inayotoka Chad hadi Darfur. Mamlaka ya Chad imekanusha.

Katika barua yake iliyotumwa siku ya Jumatatu, ujumbe wa Imarati una wasiwasi kuhusu "usambazaji wa taarifa za uongo ambazo zinadhoofisha jaribio lolote la mazungumzo ya kujenga".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.