Pata taarifa kuu
DRC-ICC-UHALIFU-USALAMA

Fatou Bensouda achunguza uhalifu dhidi ya binadamu DRC

Kiongozi wa Mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC yupo jijini Kinshasa nchini DRC, baada ya kupokea maombi ya ofisi yake kuchunguzwa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo.

Polisi wakisambaratisha maandamano yaliyoitishwa na Kanisa Katoliki DRC, Kinshasa Januari 21, 2018.
Polisi wakisambaratisha maandamano yaliyoitishwa na Kanisa Katoliki DRC, Kinshasa Januari 21, 2018. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Bensuda anakutana na viongozi wa serikali na maafisa wa Mahakama, na anatarajiwa kuzungumzia ziara yake hapo kesho.

Mwezi Januari Bunge la Umoja wa Ulaya liliomba ICC na Umoja wa Mataifa kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyokuwa vimeshuhudiwa katika jimbo la Kasai.

Wakati huo huo polisi nchini DRC imewaachilia huru wanaharakati wa Lucha waliokuwa wamekamatwa walipokuwa wanapanga kuwa na mkutano wa hadhara mjini Goma.

Wanaharakati 27 walikamatwa akiwemo kiongozi wao Rebecca Kavugho ambaye alipata tuzo kutoka Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani kama mwanamke shupavu.

Polisi wamesema wamewaachia huru wanahaharkati hao baada ya kubainika kuwa hawakuwa na kosa lolote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.