Pata taarifa kuu
BURUNDI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Burundi: uchaguzi wa urais wapangwa kufanyika Julai 15

Nchini Burundi, kalenda mpya ya uchaguzi hatimaye imekua rasmi. Jumatatu wiki hii Tume huru ya Uchaguzi (Ceni) ilipendekeza kalenda mpya ya uchaguzi. Kalenda hiyo imepitishwa na sheria ya rais, wakati ambapo vyama vikuu vya upinzani na mashirika ya kiraia vinaendelea kupinga muhula wa tatu wa rais anaye maliza muda wake Pierre Nkurunziza.

Zoezi la uchguzi Burundi.
Zoezi la uchguzi Burundi. Picha:Esdras Ndikumana/AFP
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa urais uliyokua ulipangwa kufanyika Juni 26 umeahirishwa hadi Julai 15, huku uchaguzi wa wabunge na madiwani ukipangwa kufanyika Juni 29.

Rais Pierre Nkurunziza amechukua uamzi huo, siku mbili baada ya Tume huru ya Uchaguzi (Ceni) kupendekeza kalenda mpya ya uchaguzi. Wiki mbili zilizopita wajumbe wawili wa Tume huru ya Uchaguzi kati ya watano wanaounda tuime hiyo waliitoroka nchi, na baadae wakajiuzulu kwenye nafasi zao, wakibaini kwamba hawawezi kwenda kinyume kiapo walichokula.

Jumatatu wiki hii Tume huru ya Uchaguzi (Ceni) ambayo imebaki na wajumbe watatu ilipendekeza uchaguzi wa wabunge na madiwani kuwa utafanyika Juni 25 na uchaguzi wa urais Julai 15. Siku moja baadaye Pierre Nkurunziza alisaini sheria inayowatolea wito raia kuitikia uchaguzi wa urais utakaofanyika Julai 15, huku uchaguzi wa wabunge na madiwani ukipangwa kufanyika Juni 29 badala ya juni 25 kama ilivyokua ilipendekezwa na Tume huru ya Uchaguzi.

Msemaji wa serikali ya Burundi, Philippe Nzobonariba alibaini tangu Jumatatu jioni wiki hii kwamba kinyume na tarehe hizo kuna hatari Burundi ikose taasisi halali za uongozi wa nchi, jambo ambalo halikubaliki mbele ya macho yake.
Hayo yakijiri, mazungumzo ya kisiasa kati ya upinzani, vyama vya kiraia na serikali yaliyopendekezwa na marais wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki Mei 31, hayajafanyika mpaka sasa.

“ Hii ni dharau kwa viongozi wa jumuiya ya Afrika Mashariki waliopendekeza mazungumzo ya kweli nchini Burundi “, amesema Vital Nshimirimana, kiongozi wa muungano wa mashirika ya kiraia yanayopinga muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza.

“ Hatutoshiriki uchaguzi katika mazingira hayo”, amebaini Charles Nditije kiongozi wa chama cha Uprona kisichotambuliwa na utawala wa Bujumbura. Charles Nditije ametolea wito jumuiya ya kimataifa kutosahihisha matokeo ya uchaguzi.

Wakati huo huo Askari polisi mmoja amemua kwa kumpiga risasi kijana mmoja mkazi wa mtaa wa 15 namba 1. Tukio hilo limetokea leo Jumatano mchana kweupe. Wakaazi wa wilaya ya Buyenzi wameghadhibishwa na mauaji hayo, na ndipo kuchukua uamzi wa kuzuia barabara zinazoingia na kutoka wilayani humo, kabla ya kuchoma magurudumu. Soko na maduka vimefungwa na shughuli zimesimama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.