Pata taarifa kuu
BURUNDI-MVUTANO-SIASA

Burundi: masharti kwa mazungumzo yatafautiana

Siku kumi baada ya mkutano wa kilele wa marais wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ambao walitaka uchaguzi uahirishwe kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu na mazungumzo yaanzishwe upya, wapinzani dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza na utawala , kila upande umetoa masharti yake.

Wapinzani dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza wakiandamana Bujumbura, Juni 4 mwaka 2015.
Wapinzani dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza wakiandamana Bujumbura, Juni 4 mwaka 2015. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Upinzani na mashirika ya kiraia wameomba msuluhishi katika mgogoro unaoikumba Burundi wakati huu, Saïd Djinnit, mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu, kuondolewa wakimtuhumu kuegemea upande wa utawala.

Lakini baada ya ziara fupi katika mji wa New York, Saïd Djinnit, amerejea Bujumbura, kwa mujibu wa vyanzo vya Umoja wa Mataifa, ambavyo vimebaini kwamba Umoja wa Mataifa umeendelea kuwa na imani na mjumbe wake huyo. Serikali ya Burundi ambayo hivi karibuni ilisema iko tayari kuzungumzia kuhusu muhula wa tatu, kwa sasa imebadili kauli na kusema kuwa suala la muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza halipaswi kuwekwa kwenye ajenda ya mazungumzo.

Msemaji wa serikali, Philippe Nzobonariba, ametangaza Jumanne wiki hii kwamba suala la muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza halipaswi kuwekwa kwenye “ ajenda ya mazungumzo”.

Upinzani wataka kuundwe Ceni mpya

Pande hizi mbili pia zinatofautiana kuhusu suala la Tume huru ya Uchaguzi ambayo kwa sasa imebaki na wajumbe watatu kwa jumla ya watano. Hivi karibuni wajumbe wawili wa tume hiyo waliitoroka nchi. Upinzani na mashirika ya kiraia wanabaini kwamba tume hiyo kwa sasa haitambuliwi kikatiba, na wameomba mazungumzo kuhusu Tume huru mpya ya Uchaguzi, huku wakifutilia mbali kalenda mya ya uchaguzi iliyopendekezwa na tume tume iliyoko sasa yenye wajumbe watatu. Hata hivyo serikali imekaribisha kalenda hiyo mpya ya uchaguzi

Hatimaye, serikali haijabainisha kuanzishwa upya kwa mazungumzo ya kisiasa, wakati ambapo upinzani na vyama vya kiraia wameendelea kuweka masharti mengi ili mazungumzo hayo yaanzishwe upya. Kwa upinzani, suala la awamu ya tatu "halipaswi kujadiliwa ". Kwa upande wake Frédéric Bamvuginuymvira, naibu kiongozi wa chama cha Frodebu, hatupaswi kukaa kwenye meza ya mazungumzo " ili kwenda kinyume na Katiba ya nchi na Mkataba wa mani na maridhiano wa Arusha".

" Katiba hii ilipitishwa na kura ya maoni, kwa hiyo ni mali yetu na hakuna mtu anaweza kuifanya kuwa mali yake, hata awe rais ", amesema Bamvuginyumvira.

" Mazungumzo ya kweli ni kujadili masharti ya uchaguzi uliyo wazi. Na kwa kuwa, kuna mlolongo wa masuala ya kujadiliwa, na vikwazo ambavyo vinatakiwa kuondolewa. Jumuiya ya kimataifa inahitajika kuingilia kati, katika suala nzima la maandalizi ya uchaguzi huu. Kwa sababu kama si hivyo, kuna hatari ya kutokea kwa machafuku zaidi", amesema katibu mkuu wa chama cha MSD, François Nyamoya

Mvutano umeendelea kujitokeza , huku maandamano yakiendelea katika baadhi ya wilaya za mji wa Bujumbura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.