Pata taarifa kuu
BURUNDI-CENI-UCHAGUZI-SIASA

Burundi: kalenda mpya ya uchaguzi yapendekezwa

Wajumbe wa tatu wa Tume huru ya Uchaguzi nchini Burundi (Ceni) wamekutana Jumatatu Alaasiri wiki hii na wanasiasa kutoka baadhi ya vyama vya upinzani ikiwa, ili kujadili uwezekano wa kuandaa kalenda mpya ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Burundi (Ceni), Pierre Claver Ndayicariye.
Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Burundi (Ceni), Pierre Claver Ndayicariye. DR.
Matangazo ya kibiashara

Vyama hivyo viliyoshiriki mkutano huo ni pamoja na muungano uitwao Copa, Fnl ya Jacques Bigirimana na Uprona ya Concilie,

Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi nchini Burundi, Pierre-Claver Ndayicariye amependekeza kuwa uchaguzi wa wabunge na madiwani ufanyike Juni 26 mwaka 2015.

Pierre-Claver Ndayicariye pia amependekeza kuwa uchaguzi wa rais ufanyike Julai 15 na ule wa maseneta ufanyike Julai 24 mwaka 2015.

Edouard Nduwimana, waziri wa Burundi mwenye dhamana ya mambo ya ndani.
Edouard Nduwimana, waziri wa Burundi mwenye dhamana ya mambo ya ndani. assemblee.bi

Waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana, ambaye ameshiriki mkutano huo, amebaini kwamba hati za kukamatwa kwa watu walioandaa maandamano zitafutwa kama maandamano yatasitishwa mara moja.

Hata hivyo zaidi ya vyama vikuu 17 vya upinzani ikiwa ni pamoja na muungano wa vyama vya upinzani Adc Ikibiri, muungano wa wanasiasa wanaojitegemea (Amizero y'abarundi) unaoongozwa na Agathon Rwasa, Frodebu Nyakuri, MSD, UPD na vinginevyo vimesusia mkutano huo.

Vyama hivyo vimebaini kwamba Tume ya huru ya Uchaguzi (Ceni) haipo baada ya wajumbe wake wawili kujiuzulu juma lililopita.

“ Hatuwezi kuitishwa na taasisi ambayo haipo ”, Charles Nditije kutoka muungano wa wanasiasa wanaojitegemea (Amizero y'Abarundi) amesema kwa niaba ya vyama vikuu 17 vya upinzani.

Katiba ya Burundi inaeleza kwamba Tume huru ya Uchaguzi (Ceni) inaundwa na wajumbe wa tano. Wajumbe hao wanateuliwa na sheria ya kirais na kupitishwa na baraza mbili za Bunge na Seneti kwa wingi wa robo tatu za wabunge na maseneta, kila baraza upande wake.

" Wakati ambapo wajumbe wawili wa Tume huru ya Uchaguzi wamejiuzulu ni marufuku kwa tume hiyo kuchukua uamzi wowote ", amesema Charles Nditije, huku akibaini kwamba kwa sasa tume hiyo haitanbuliwi kikatiba.

Kiongozi wa chama cha Uprona kisiyotambuliwa na sereikali ya Bujumbura, Charles Nditije (katikati), akizungukwa na wafuasi wake huku akizuliwa na polisi
Kiongozi wa chama cha Uprona kisiyotambuliwa na sereikali ya Bujumbura, Charles Nditije (katikati), akizungukwa na wafuasi wake huku akizuliwa na polisi RFI/Esdras Ndikumana

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.