Pata taarifa kuu
BURUNDI-UN-SIASA-USALAMA

Burundi: Upinzani waomba mpatanishi mpya katika Umoja wa Mataifa

Vyama 17 vya upinzani nchini Burundi vimesema havina tena imani na mjube maalumu wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Said Djinnit, na kuomba mpatanishi mpya katika Umoja wa Mataifa.

Saïd Djinnit, msuluhishi wa Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu.
Saïd Djinnit, msuluhishi wa Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu. AFP/SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Vyama vya upinzani nchini Burundi vimemtuhumu mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa maziwa makuu Said Djinnit ambae ni mpatanishi wa mgogoro wakisiasa uliopo kwa kuegemea upande mmoja na kuomba kuteuliwa kwa mpatanishi mwingine katika mazungumzo na serikali ya rais Pierre Nkurunziza.

Vyama hivyo vinamkosoa Djinnit kuwasilisha ripoti yake kwa marais wa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki mjini Dar es Salaam juma lililopita bila ya kuwashirikisha kwa kile kilichoandikwa katika ripoti hiyo.

Hata hivyo Said Djinnit amehakikisha kuwa bado hajaona waraka huo uliyowasilishwa na upinzani kwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

 

Wakati hayo yakijiri, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani mwenye dhamana ya Demokrasia na Haki za Binadamu, Tom Malinowski aliyemaliza ziara yake nchini Burundi amemtaka rais Pierre Nkurunziza kutogombea muhula wa tatu jambo ambalo amesema ni kinyume na makubaliano ya Arusha.

Sanjari na hayo, Umoja wa Mataifa umetoa wito Alhamisi wiki hii wa kuwapokonya silaha haraka iwezekanavyo vijana wa chama tawala maarufu kama Imbonerakure ili kuruhusu maandalizi ya uchaguzi ulio huru, wa haki na wa amani nchini Burundi. Kutangaza kuwania muhula wa 3 kwa rais Nkurunziza kumeendelea kuzua ghasia nchini humo ambapo watu zaidi ya 30 wamepoteza maisha katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.