Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Wabunge wa Uingereza waunga mkono uchaguzi wa mapema wa Desemba 12

Wabunge wa Uingereza wamepiga kura Jumanne wiki hii na kupitisha mpango wa Waziri Mkuu Boris Johnson wa kufanyika kwa uchaguzi wa mapema wa wabunge tarehe 12 Desemba ili kuondokana na mchakato wa Brexit ambao umekwamisha mambo mengi nchini Uingereza kwa zaidi ya miaka mitatu.

Wabunge wa Uingereza wakipiga kura na kuipitisha mpang wa Boris Johnson wa kufanyika kwa uchaguzi wa mapema wa Desemba 12, Oktoba 29, 2019.
Wabunge wa Uingereza wakipiga kura na kuipitisha mpang wa Boris Johnson wa kufanyika kwa uchaguzi wa mapema wa Desemba 12, Oktoba 29, 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya saa kadhaa za majadiliano yenye mvutano mkubwa, hatimaye wabunge walipitisha mpango huo kwa idadi kubwa ya kura 438 dhidi ya 20 kwa kufanyika uchaguzi wa mapema uliopendekezwa na Boris Johnson.

Nakala hiyo bado inatarajiwa kupitishwa Jumatano wiki hii Bunge la Seneti.

Kwa hatu hiyo Bunge linatazamiwa kufutwa Jumatano ijayo saa 00:01 usiku (saa za kimataifa), amesema waziri mwenye dhamana ya uhusiano na Baraza la Wawakilishi, Jacob Rees-Mogg.

Ilikuwa jaribio la nne la Boris Johnson kuitisha uchaguzi wa mapema, mpango ambao amefanikiwa kwa msaada mkubwa wa chama kikuu cha upinzaji cha Labour.

- Chaguzi tatu ndani ya kipindi cha miaka minne

Uhaguzi huu Mkuu, uliopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka 2022, utakuwa wa tatu ndani ya kipindi cha miaka minne, baada ya kura ya maoni ya mapema mwaka 2017, na mchakato wa Brexit wenye utata mkubwa, miaka miwili baada ya ule wa maka 2015.

Kawaida chaguzi zote zilizotangulia zilifanyika katika majira ya Joto, Uchaguzi huu Mkuu pia utakuwa wa kwanza kufanyika mwezi Desemba tangu mwaka 1923.

Kabla ya kupoitishwa kwa mpango huo, kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour nchini Uingereza Jeremy Corbyn, amliwaambia wabunge wenzake kwamba ataunga mkono uchaguzi wa mapema nchini humo kwa kuwa sasa uwezekano wa kuondoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano haupo. Kauli ya kiongozi huyo wa chama cha upinzani ilikuja saa chache tu baada ya waziri mkuu Boris Johnson kujiandaa kuwaomba wabunge kwa mara ya nne kuidhinisha uchaguzi wa mapema akisema wapiga kura wanapaswa kupewa nafasi ya kuuvunja mkwamo wa Brexit katika bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.