Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Wabunge wa Uingereza waanza mazungumzo ya siku tano kuhusu Uingereza kujitoa EU

Serikali ya Uingereza, huenda ilivunja taratibu za bunge, kwa kutochapisha ushauri wa kisheria, kuhusu mkataba wa nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Westminster Palace, Makao makuu ya Bunge la Uingereza London.
Westminster Palace, Makao makuu ya Bunge la Uingereza London. David Castor/Palais de Westminster Londres Parlement
Matangazo ya kibiashara

Spika wa bunge John Bercow, ametoa uamuzi huo na kusema, sasa wabunge watajadili suala hilo na kulipigia kura Jumanne wiki hii.

Hii inaamanisha kuwa, huenda wabunge wakachelewa kuanza kujadili na kupigia kura mkataba wa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, uliopendekezwa na Waziri Mkuu Theresa May, mkataba amaboa wabunge wengi wameonekana kuupinga.

Mwezi uliyopita Umoja wa Ulaya uliunga mkono makubaliano ya Uingereza kujitenga na umoja huo, haua mabayo inafungua njia kwa taifa hilo kuanza safari ya kujitenga rasmi.

Viongozi hao waliokutana Novemba 25, 2018 waliafikiana kwa pamoja Uingereza kujitoa katika umoja huo ifikapo mwaka 2019.

Uingereza inakuwa nchi ya kwanza katika historia ya Umoja wa Ulaya (EU) kujitoa kwenye muungano huo wenye nchi wanachama 28.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.