rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Sudani Kusini UNSC Marekani Salva Kiir

Imechapishwa • Imehaririwa

UNSC: Azimio dhidi ya Sudan Kusini kupigiwa kura

media
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa UN Photo/Loey Felipe

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baadaye siku ya Alhamisi, linatarajiwa kujadili na kupigia kura azimio la kuiwekea vikwazo Sudan Kusini kununua silaha kutoka nje ya nchi.


Azimio hili limeandaliwa na Marekani ambayo imesema ni kutokana na hatua ya serikali ya Sudan Kusini inayoongozwa na rais Salva Kiir, kuendeleza vita nchini humo.

Watu mashuhuri wanaominiwa kuendelea kuchochea vita ambavyo vilianza mwaka 2013, miaka miwili baada ya taifa hilo kupata uhuru kwa kujitenga na Sudan.

Washington DC inasema ili kumaliza vita ambavyo vimesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na mamilioni kuyakimbia makwao, ni sharti uamuzi huo uchukuliwe.

Aidha, Marekani imewashtumu viongozi wa Juba kwa kuvunja mara kwa mara mikataba ya amani inayokubaliwa jijini Addis Ababa kati ya serikali na waasi ili kumaliza mapigano hayo.

Azimio hilo pia linatarajiwa kuwaongezea wanajeshi wa Umoja wa Matafa nchini humo UNMISS kuendelea kuwepo kwa mwaka mmoja zaidi.

Kikosi hicho cha wanajeshi 12,500 kinapiga kambi jijini Juba kwa lengo la kuwalinda raia, hatua iliyochukuliwa mwaka 2016 baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya vikosi vya rais Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar.

Kura tisa kutoka wajumbe 15 wa Baraza hilo zinahitajika ili azimio hilo kupitishwa.

Tayari China, Urusi na Ethiopia zimesema hazitaunga mkono azimio hilo.

Rais Kiir, hivi karibuni alinukuliwa akiilaani mpango huo wa Marekani kuwasilisha azimio hilo.