Pata taarifa kuu
Ufaransa

Rais Hollande asema uchaguzi wa Marekani hautadhoofisha uhusiano wa Marekani na Umoja wa Ulaya

Rais wa Ufaransa Francois Hollande leo Jumamosi amesema kuwa ana matumaini kwamba vyovyote matokeo ya uchaguzi urais wa mwaka huu nchini Marekani yatakavyokuwa hayata dhoofisha mahusiano ya Marekani na Umoja wa Ulaya.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande akizungumza wakati wa mkutano wa kilele wa NATO, July 9, 2016.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande akizungumza wakati wa mkutano wa kilele wa NATO, July 9, 2016. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika mkutano wa Kilele wa umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO jijini Warsaw, Rais Hollande amesema ushirikiano wa mataifa yanayotumia bahari ya Atlantic ni muhimu sana, na uchaguzi wa Marekani hautakiwi kuhatarisha mahusiano Haya,

Rais Hollande amesema kuwa wanahitaji mahusiano hayo kwa ajili ya amani na usalama.

Mwezi Juni, rais Hollande alisema kuwa ushindi unaotazamiwa wa mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump unge teteresha mahusiano kati ya Ulaya na Marekani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.