Pata taarifa kuu
IMF

Mkurugenzi wa IMF asema kunadalili ya mzozo wa kiuchumi kumalizika barani Ulaya

Mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF, Christine Lagarde amesema kuwa kwasasa mdororo wa kiuchumi kwenye ukanda wa Jumuiya ya Ulaya huenda ukapata suluhisho na kumalizika kabisa. 

Mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF Christine Lagarde
Mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF Christine Lagarde © Reuters/Stephen Jaffe
Matangazo ya kibiashara

Lagarde ameyasema hayo kufuatia hapo jana wakopeshaji binafsi nchini Ugiriki kuipatia mkopo nchini ya Ugiriki ambayo sasa kuna uwezekano mkubwa nchi hiyo kuondokana na matatizo ya kiuchumi.

Siku ya Alhamisi ndio ilikuwa siku ya mwisho kwa wakopeshaji binafsi kuhakikisha wanaipatia Ugiriki mkopo miwngine wa fedha, mpango ambao awali wakopeshaji hao walitishia kusogeza muda mbele kwakile walichoeleza kuwa ni wasiwasi wa serikali hiyo kutumia mkopo huo.

Kiongozi huyo amesema kuwa kwa hali inavyoonekana hivi sasa, ni wazi kuwa nchi ya Ugiriki itaondokana na madeni makubwa ambayo yanaikabili na kwamba matatizo ya kicuhumi yatapatiwa ufumbuzi kutokana na mkopo ambao wamepatiwa.

IMF na Umoja wa Ulaya EU waliipatia Ugiriki kiasi cha Euro bilioni 130 kama fedha za mkopo kwaajili ya kulipa madeni na matumizi mengine ya ndani ambayo yatasaidia kufufua uchumi wa nchi hiyo.

Licha ya kupongeza hatua ambayo nchi ya Ugiriki imechukua ya kubana matumizi kwa kiasi cha juu, Lagarde ameendelea kuzionya nchi nyingine kutofanya matumizi makubwa ya ndani hali ambayo itapelekea kutumbukia tena kwenye mdororo wa uchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.