Pata taarifa kuu
Serbia-EU

Jenerali Ratko Mladic afikishwa mahakamani

Jenerali Ratko Mladic ambaye Rais wa Serbia Boris Tadic alitangaza kukamatwa kwake nchini Serbia  Alhamisi, Mei 26 mwaka 2011 baada ya kutafutwa katika kipindi cha miaka 6 hatimaye amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji zinazomkabili.Hata hivyo hali ya afya yake ndiyo itaamua kama ataendelea kuhudhuria katika shauri lake na taarifa ya madaktari inasubiriwa kwa hamu kuamua hatma yake kwani kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa kwa juma zima mfululizo. 

Getty Images/Jason Gold
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya hapo waziri wa mambo ya ndani alikuwa ametangaza kukamatwa kwa mtu ambaye alionekana kufanana na jenerali Mladic.

Jenerali huyo wa zamani anatuhumiwa kwa makosa ya mauaji ya kimbari na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita uliotendeka nchini Yougoslavia (TPIY) baada ya kuwateketeza raia Waislam wa Bosnia mwaka 1995 mjini Srebrenica mashariki mwa Bosnia.

“Ratko Mladic amekamatwa leo asubuhi mapema” amesema Rais wa Serbia wakati polisi imesema,“ tunafanya vipimo vya DNA” . Mtu aliyekamatwa ana vitambulisho vya Milorad Komadic, na siri za kukamatwa kwake zilitolewa na mchunguzi ambaye hakutaja jina lake, kama ilivyotangaza wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo.

Boris Tadic amethibitisha kuwa Ratko Mladic amekamatwa “katika ardhi ya Serbia” bila hata hivyo kufafanua eneo alipokamatwa. Taratibu za kumpeleka mahakamani Hague kwenye makao makuu ya mahakama hiyo ya kimataifa kuhusu makosa ya Yugoslavia zinaelekea kukamilika.

Kukamatwa kwa jenerali huyo ni moja kati ya masharti yaliotolewa na Umoja wa Ulaya kwa Serbia kabla ya kuikubalia kuwa mwanachama wa umoja huo. Kukamatwa huko ni  ”Matokeo ya ushirikiano mwema baina ya Serbia na mahakama ya Hague. Leo tunaufungua ukurasa mpya wa historia ya ukandaa huu ambao utatupeleka katika maridhiano ya kudumu” ya kikanda, amesisitiza Rais Boris Tadic.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.