Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Urusi inakubali kwa mara ya kwanza kwamba iko 'katika hali ya vita'

Urusi iko "katika hali ya vita" dhidi ya Ukraine, msemaji wa Kremlin amekiri katika mahojiano yaliyochapishwa Ijumaa Machi 22, baada ya kusisitiza kutangaza shambulio dhidi ya jirani yake, lililoanzishwa miaka miwili iliyopita, kama "operesheni maalum" na akafutilia mbali matumizi ya neno "vita".

Dmitry Peskov, msemaji wa Kremlin.
Dmitry Peskov, msemaji wa Kremlin. via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

"Tunajikuta katika hali ya vita. Ndio, ilianza kama operesheni maalum ya kijeshi, lakini mara tu genge hili lote lilipoundwa, wakati nchi za Magharibi zilishiriki katika haya yote pamoja na Ukraine, kwetu imekuwa vita. Nina hakika na hili na kila mtu lazima aelewe hili," amesema Dmitri Peskov katika mahojiano na vyombo vya habari vya "Argoumenty I Fakty".

Hii sio mara ya kwanza kwa Kremlin kutumia neno hili. Mnamo mwezi wa Desemba 2022, kisha mwezi wa Februari 2023, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema maneno haya, akisema: “Ni [nchi za Magharibi] zilizoanzisha vita hivi, na tulitumia nguvu kukomesha. "

Kwa Warusi wengine wote na wageni wanaoishi nchini Urusi - ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari - matumizi ya neno "vita" hadharani kuhusu "operesheni maalum" nchini Ukraine ni uhalifu unaoweza kuadhibiwa kwa kifungo cha hadi miaka kumi na tano jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.