Pata taarifa kuu

EU kupendekeza kufunguliwa kwa mazungumzo ya kujiunga na Bosnia Herzegovina

Miaka ishirini na tisa baada ya kumalizika kwa vita, Tume ya Ulaya inajiandaa kupendekeza kufunguliwa kwa mazungumzo ya kujiunga na Bosnia Herzegovina. Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia kwa hivyo itakuwa nchi ya mwisho ya Balkan kuweza kuanza mazungumzo ya kujiunga na Umoja wa Ulaya (EU), baada ya kupewa hadhi ya kuwa nchi inayogombea mnamo 2022. Hata kama hali ya kisiasa ya ndani inaendelea kuwatia wasiwasi viongozi wa chi za Umoja wa Ulaya.

Majadiliano kati ya wawakilishi wa Umoja wa Ulaya na maafisa wa Bosnia, Novemba 1, 2023, mjini Sarajevo.
Majadiliano kati ya wawakilishi wa Umoja wa Ulaya na maafisa wa Bosnia, Novemba 1, 2023, mjini Sarajevo. © Armin Durgut / АР
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Brussels, Pierre Benazet

Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, amesema siku ya Jumanne kwamba Bosnia Herzegovina imepata maendeleo zaidi katika mwaka mmoja kuliko katika miaka kumi iliyopita kwenye njia yake ya kuelekea uanachama. Tume inachapisha ripoti ya upanuzi wa Muungano, ambapo inathibitisha kwamba katika mambo matano muhimu, "nchi inaonyesha kwamba inaweza kuheshimu vigezo vya kujiunga".

Kwanza, kuna mapambano dhidi ya utakatishaji fedha haramu na ufadhili wa ugaidi, uboreshaji wa usimamizi wa wimbi la wahamaji, pia uboreshaji wa programu za mazungumzo na upatanisho, kisha kuingizwa katika rekodi za uhalifu za kitaifa hukumu za Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa Yugoslavia ya zamani.

Kuingiliana na sera ya kigeni na usalama

Kwa mujibu wa Tume, zaidi ya yote kuna uwiano wa Bosnia na sera ya pamoja ya mambo ya nje na usalama ya Muungano. Lakini katika suala hili, wasiwasi wa Ulaya umeonyeshwa wazi katika siku za hivi karibuni na ziara za mfululizo huko Sarajevo na mawaziri wa mambo ya nje wa Italia, Austria na Ujerumani.

Hawakujizuia katika ukosoaji wao kwa matamshi ya Rais wa Waserb wa Bosnia Milorad Dodik ya kuunga mkono Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.