Pata taarifa kuu

Putin ameapishwa kuiongoza Urusi kwa muhula mwengine wa miaka sita

Raisi wa Urusi Vladimir Putin ameapishwa kuongoza nchi yake kwa kipindi kingine cha miaka sita baada yake kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu wa urais wa mwezi Machi mwaka huu.

Rais Putin sasa atawaongoza raia wa Urusi kwa kipindi cha miaka sita.
Rais Putin sasa atawaongoza raia wa Urusi kwa kipindi cha miaka sita. via REUTERS - Kremlin.ru
Matangazo ya kibiashara

Putin mwenye umri wa miaka 71, atawaongoza Warusi kwa muhula wake wa tano sasa.

Katika hotuba yake baada ya kuapishwa, Putin amewaeleza raia wa nchi yake kuwa wataibuka washindi baada ya kipindi kigumu.

Kiongozi huyo anatarajiwa kuiongoza nchi yake kwa mara nyengine tena baada ya kukabiliwa na masuala mabalimbali ikiwemo kuwanyamazisha wapinzani wake pamoja na kuivamia nchi jirani ya Ukraine katika kipindi cha muhula wake wa nne.

Rais Putin wakati wa hotuba yake fupi ameapa kuilinda nchi yake
Rais Putin wakati wa hotuba yake fupi ameapa kuilinda nchi yake AFP - ALEXEY MAISHEV

Putin kwa sasa ndiye rais ambaye ameiongoza nchi yake kwa kipindi kirefu zaidi tangu uongozi wake Josef Stalin, ambapo sasa ataongoza Urusi hadi mwaka wa 2030.

Katika hafla iliohudhuria na watu wachache mashuhuri, kiongozi huyo pia ameapa kuilinda nchi yake.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa Putin ameisaidia nchi yake pakubwa katika masuala ya kiuchumi tangu kuchukua uongozi kutoka kwa rais Boris Yeltsin mwaka wa 1999.

Hafla ya kuapishwa kwa rais Putin imehudhuria na watu wachache wenye umaarufu
Hafla ya kuapishwa kwa rais Putin imehudhuria na watu wachache wenye umaarufu via REUTERS - Sergei Savostyanov

Tangu kuivamia nchi ya Ukraine mwaka wa 2022 katika vita ambavyo vimegeuka kuwa vikubwa zaidi barani Ulaya tangu vita vya pili vya dunia, Urusi imekabiliwa na vikwazo vikubwa kutoka kwa nchi za Magharibi.

Soma piaPutin kutawazwa kama rais wa Urusi kwa muhula wa tano

Kutokana na vikwazo hivyo, Urusi imeonekana kutafuta washirika wapya kutoka nchi za China, Iran na Korea kaskazini kwa uungwaji mkono na ushirika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.