Pata taarifa kuu

Uingereza yawawekea vikwazo Waserbia 2 wa Bosnia kwa kuhatarisha usalama

London imechukuwa vikwazo dhidi ya viongozi wawili wa Waserbia wa Bosnia, Milorad Dodik na Zeljka Cvijanovic. Wanashtumimiwa kwa kuhatarisha usalama wa nchi chini ya ushawishi wa Moscow. Vikwazo hivi viliamuliwa miezi mitatu baada ya vile vilivyowekwa na Washington kwa sababu kama hiyo.

Milorad Dodik, afisa wa Serbia katika ofisi ya rais ya Bosnia ya pande yatu aliwekewa vikwazo siku ya Jumatatu Aprili 11 na Uingereza, akishutumiwa kuhatarisha usalama wa nchi hiyo chini ya ushawishi wa Moscow.
Milorad Dodik, afisa wa Serbia katika ofisi ya rais ya Bosnia ya pande yatu aliwekewa vikwazo siku ya Jumatatu Aprili 11 na Uingereza, akishutumiwa kuhatarisha usalama wa nchi hiyo chini ya ushawishi wa Moscow. © Associated Press
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo lilitolewa na vyombo vya habari na kuchapishwa kwenye tovuti ya serikali ya Uingereza. Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje Liz Truss, viongozi hao wawili wa Waserbia wa Bosnia, Milorad Dodik, afisa wa Serbia katika ofisi ya rais ya Bosnia ya pande yatu na Zeljka Cvijanovic, walitatiza kwa makusudi amani iliyokuwa imepatikana kwa bidii huko Bosnia-Herzegovina. Waziri huyo pia ameongeza kuwa tabia zao, “zinazotiwa moyo na Rais Putin; zilitishia utulivu na usalama wa raia wa mataifa ya balkan".

Tangu kumalizika kwa vita vya Bosnia, vilivyoua karibu watu 100,000 kati ya mwaka 1992 na 1995, nchi hiyo imegawanyika katika kambi mbili chini ya Mkataba wa Amani wa Dayton, Jamhuri ya Serbia na Shirikisho la Waislamu wa Croatia, lililounganishwa na serikali kuu. Lakini katika miezi ya hivi karibuni, mvutano umekuwa ukiongezeka na Milorad Dodik, ambaye anajaribu kuipa Jamhuri ya Serbia ya Bosnia haki yake, mamlaka yake ya kodi na jeshi lake, na kuibua hofu ya kuvunjika kwa nchi hii, au hata kuzuka kwa mgogoro mpya.

Viongozi hao wawili kwa hivyo mali zao zitazuiliwa nchini Uingereza na kupigwa marufuku kingia katika ardhi ya Uingereza. Kwa vikwazo hivi, Waziri wa Mambo ya Nje anasema anataka kuonyesha kwamba maadui wa amani watawajibishwa kwa hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.