Imetimia miaka mwili tangu Urusi ilipoivamia Ukraine
Nairobi – Tarehe 24 ya mwezi Februari mwaka wa 2022, Urusi ilitekeleza uvamizi nchini Ukraine, ikianzisha vita vikubwa zaidi barani Ulaya tangu vita vya pili vya dunia.
Imechapishwa:
Miaka miwili baadae, bado hakujaonekana matumaini ya kumalizika kwa mapigano hayo.
Wachambuzi wa masuala ya kimataifa wanasema kuwa mwaka huu wa 2024 utashuhudia makabiliano makali, Ukraine ikitarajia kuchukua maeneo yake yanayokaliwa na Urusi.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kupitia mtandao wake wa X, ameeleza kuwa nchi yake haitachoka kuiiunga mkono Ukraine katika vita vyake na Urusi.
Ukraine imeapa kupata ushindi dhidi ya uvamizi wa Urusi katika ardhi yake wakati huu vita hivyo vikiingia katika mwaka wake wa pili.
Dear great people of a great country, I am immensely proud of each of you. I admire each one of you. I believe in each one of you. Any normal person wants the war to end. But none of us will allow Ukraine to end.
— Volodymyr Zelenskyy / Володимир Зеленський (@ZelenskyyUa) February 24, 2024
That is why when it comes to ending the war, we always add: on our… pic.twitter.com/MQttTK8Ex2
Hatua ya Kyiv kujilinda dhidi ya mashambulio ya Moscow imeonekana kulemazwa na ukosefu wa usambazaji wa silaha inazohitaji kutoka kwa washirika wake nchi za Magharibi.
Wakuu wa nchi za G7 wanatarajiwa kukutana kwa njia ya mtandaoni kuadhimisha miaka miwili ya vita hivyo, rais Volodymyr Zelensky akiwa miongoni mwa watakaohudhuria.
Waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni ni miongoni wa washirika wa Kyiv ambao wamewasili nchini Ukraine kwa maadhimisho ya miaka mwili ya vita, akitarajiwa kuongoza kikao cha mtandaono cha wakuu wa G7.
Tayari nchi ya Uingereza imetangaza msaada wa Euro milioni 245 kwa nchi ya Ukraine kuisaidia kupata silaha inazohitaji kwa dharura.