Pata taarifa kuu

Zelensky afanya ziara ya kushtukiza NATO ili kuhakikisha msaada kutoka kwa washirika wake

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky siku ya Jumatano amewataka wanachama wa NATO kuongeza uungaji wao mkono kwa nchi yake wakati msimu wa baridi unakaribia, ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kwanza katika makao makuu ya Muungano huo tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (kushoto) na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakiwa katika mkutano wa NATO.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (kushoto) na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakiwa katika mkutano wa NATO. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tunahitaji kuungwa mkono na viongozi, ndiyo maana niko hapa," amesema Bw. Zelensky ambaye alisema siku moja kabla kwamba alikuwa na wasiwasi kuhusu matokeo ya mchango wa washirika katika nchi yake katika vita kati ya Israel na Hamas, baada ya shambulio lililozinduliwa Jumamosi na vuguvugu la Waislam wa Palestina kutoka Gaza. Bwana Zelensky alishiriki katika mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa NATO, ikiwa ni sehemu ya ziara ya ghafla.

"Wapendwa marafiki, lazima tushinde vita vya msimu wa baridi dhidi ya ugaidi," ametangaza mbele ya nchi wanachama wa kundi la Ramstein, ambalo lilichukua jina hilo kutoka kambi ya wanajeshi wa Marekani iliyoko nchini Ujerumani ambapo nchi hizi zilikutana kwa mara ya kwanza ili kuratibu msaada wao wa kijeshi kwa Ukraine.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, ambaye nchi yake ndiyo mchangiaji mkuu wa juhudi za vita vya Ukraine, ametaka kumtuliza moyo rais wa Ukraine mwanzoni mwa mkutano huo. "Tuko hapa kutoa kile kinachohitajika, kwa muda muafaka," amesema.

Ametangaza msaada mpya wa kijeshi wa Marekani unaofikia dola milioni 200 kwa Ukraine katika mfumo wa mifumo ya ulinzi ya anga, hitaji muhimu kwa Ukraine kabla ya majira ya baridi. Msaada huu utaleta jumla ya msaada wa kijeshi wa Marekani kufikia dola milioni 43.9, amebainisha.

Majira ya baridi yaliyopita, Urusi ililenga miundombinu ya nishati ya Ukraine, na kuwanyima mara kwa mara raia umeme.

Hali ambayo Kyiv na washirika wake hawataki kuiona tena. Msisitizo utawekwa kwenye "ngao ya msimu wa baridi" ya ulinziw anga, ili kupata funzo kwa yale yalitotokea mwaka jana, mwanadiplomasia  katika NATO alisema wiki hii. "Ulinzi dhidi wa anga ni sehemu muhimu ya mwitikio," amesema Bw. Zelensky, akiwashukuru washirika wake kwa msaada ambao tayari wamepokea. "Jinsi tutakavyoishi msimu huu wa baridi ni muhimu kwetu," amesisitiza.

Bwana Zelensky amekaribishwa na Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, ambaye pia ametaka kumhakikishia kuhusu dhamira ya Washirika ambao wengine wanahofia kuiona ikidhoofika baada ya siku zisizopungua 600 za vita. "Vita vyenu ni vita vyetu, usalama wenu ni usalama wetu," amesema Bw. Stoltenberg akiambatana na Rais Zelensky.

"Uangalifu wa kimataifa unahatarisha kuiacha Ukraine, na hiyo itakuwa na athari," kiongozi wa Ukraine alionya siku moja kabla kwenye kituo cha televisheni cha Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.