Pata taarifa kuu

Joe Biden: Msaada kwa Kyiv uko hatarini kufuatia mgogoro wa kisiasa Marekani

Rais wa Marekani Joe Biden ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea huko Washington, akibaini kwamba unatishia msaada wa Marekani kwa Ukraine.

Joe Biden amesema Washington ilizileta pamoja nchi zaidi ya 50 ili kuisaidia Ukraine na kwamba kwa sasa wanao uwezo wa kufadhili "msaada ujao" akisisitiza kuwa zipo "njia zingine" za kupata pesa, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.
Joe Biden amesema Washington ilizileta pamoja nchi zaidi ya 50 ili kuisaidia Ukraine na kwamba kwa sasa wanao uwezo wa kufadhili "msaada ujao" akisisitiza kuwa zipo "njia zingine" za kupata pesa, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi. AP - Manuel Balce Ceneta
Matangazo ya kibiashara

Bunge la Marekani linatarajiwa kuidhinisha bajeti ya mwaka ujao ambayo Ikulu ya White House inatarajia kuwa itajumuisha pia msaada mpya kwa Ukraine wa dola bilioni 24,  ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Ukraine kukabiliana na uvamizi wa Urusi..

Hata hivyo, utawala wa Biden unakabiliwa na tatizo kubwa kwa kuwa Wabunge wa mrengo mkali wa kulia wanapinga vikali msaada huo kwa Ukraine, jambo lililochangia pia kuondolewa katika wadhifa wake, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Kevin McCarthy.

Siku ya Alhamisi, Biden atakutana na washauri wake wa karibu wanaohusika na masuala ya usalama wa taifa akiwemo mkuu mpya wa majeshi, ili kujadili miongoni mwa mambo mengine, suala hili la msaada kwa Ukraine.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Biden amesisitiza kuwa ushindi wa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi, ni kwa maslahi ya Marekani na washirika wake.

Joe Biden amesema Washington ilizileta pamoja nchi zaidi ya 50 ili kuisaidia Ukraine na kwamba kwa sasa wanao uwezo wa kufadhili "msaada ujao" akisisitiza kuwa zipo "njia zingine" za kupata pesa, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.