Pata taarifa kuu

Mataifa mbalimbali barani Ulaya yanakabiliwa na viwango vya juu vya joto

Nairobi – Nchi mbalimbali barani Ulaya na huko Amerika Kaskazini, zinashuhudia kiwango kikubwa cha joto, huku kukishuhudiwa kwa majanga ya moto ya nyika.

Mataifa mbalimbali barani Ulaya yanakabiliwa na joto kubwa wakati huu moto wa nyika pia ikishuhudiwa katika baadhi ya nchi
Mataifa mbalimbali barani Ulaya yanakabiliwa na joto kubwa wakati huu moto wa nyika pia ikishuhudiwa katika baadhi ya nchi © AFP / FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Nchini  Ugiriki, watu 18 wanaoaminiwa kuwa wahamiaji, wamepatikana wameuwa msituni Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo baada ya kuteketezwa na moto wa nyika.

Ripoti zinasema, miili hiyo ilipatikana karibu na mbunga ya wanyama ya Dadia, inayopakana na Uturuki.

Nchini Marekani kwa karibu wiki mbili sasa, jimbo la Hawaii pia limeshuhudia, kuteketea kwa misitu katika kisiwa cha Maui na kusababisha zaidi ya watu 100 kupoteza maisha.

Huko Canada, moto huo umeendelea kuwahangaisha Magharibi mwa nchi hiyo huku eneo lenye ekari Milioni 15 ikiteketea.

Mbali na majanga haya ya moto, mataifa kadhaa ya bara Ulaya, ikiwemo Ufaransa, inashuhudia kiwango kikubwa cha joto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.