Pata taarifa kuu
USALAMA MAJINI

Ugiriki: Zoezi la kutafuta miili ya watu linaendelea baada ya kuzama kwa boti la wahamiaji

Tukio hili linaweza kuwa mojawapo mbaya zaidi kwenye njia wanayotimia wahamiaji katika Mediterania ya Kati na mojawapo ya matukio mabaya zaidi duniani. Karibu miili 80 imetolewa kutoka kwa maji, lakini idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo inaweza kuwa ya juu zaidi. Mamlaka ya Ugiriki imetangaza siku tatu za maombolezo.

Wahamiaji waliookolewa katika bahari ya wazi nje ya Ugiriki, baada ya boti yao kupinduka, wanasimama nje ya ghala linalotumika kama makazi, kwenye bandari ya Kalamata, Ugiriki, Juni 15, 2023.
Wahamiaji waliookolewa katika bahari ya wazi nje ya Ugiriki, baada ya boti yao kupinduka, wanasimama nje ya ghala linalotumika kama makazi, kwenye bandari ya Kalamata, Ugiriki, Juni 15, 2023. © Stelios Misinas / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Athenes, Eric de Lavarène

Kulingana na mahirika kadhaa yasiyo ya kiserikali, ambayo yaliwasiliana na boti hiyo, hadi watu 750 walikuwa ndani ya boti hiyo. Takriban watu zaidi ya mia moja waliokolewa. Baadhi katika hali ya juu ya hypothermia. Inaaminika kuwa oti hiyo iliyumbayumba kabla ya kuzama katika moja ya sehemu zenye kina kirefu zaidi katika bahari ya Mediterania, karibu na rasi ya Peloponnese nchini Ugiriki. Usiku kucha, msako uliendelea kujaribu kutafuta manusura. Meli hiyo inaonekana ilikuwa imejaa kupita kiasi. Mashirika yasio ya kiserikali yanataja watu 400 hadi 750 waliokuwa kwenye boti hiyo. Hakuna aliyekuwa amevaa koti la uokoaji.

Baharini kwa siku nne

Boti hiyo ilikuwa ikitokea Tobruk, mashariki mwa Libya, na ilikuwa ikielekea pwani ya Italia. Ilikuwa imekaa baharini kwa siku nne na inaonekana hakukuwa na maji wala chakula tena. Walinzi wa pwani ya Ugiriki wanadai walikuwa na mawasiliano saa chache kabla na boti hiyo. Lakini wahamiaji hao waliripotiwa kukataa msaada wao. Hata hivyo, mashirika kadhaa ya kiutu yanawashtumu kwa kutoingilia kati kutokana na hali ya boti hiyo. Mfanyakazi wa kujitolea anayefanya kazi na laini ya Simu ya Alarm Phone, ambayo hupokea simu za shida kutoka kwa wahamiaji, anasema tahadhari ya kwanza ilitolewa muda mrefu kabla. simu hiyohaikujibiwa.

Mamlaka ya Ugiriki inahusishwa mara kwa mara na tabia ya kufurusha wahamiaji kinyume na sheria ambao meli zao zinarudishwa kwenye maji ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.