Pata taarifa kuu

Watu watatu wameuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani Odesa Ukraine

Watu watatu wameuawa  mapema Jumamosi katika moto uliosababishwa na vifusi vilivyoanguka kutoka kwa ndege zisizo na rubani katika eneo la Odesa kusini mwa Ukraine, maofisa wa eneo hilo wamesema.

Watu watatu wameripotiwa kuawaua Odesa Ukraine katika shambulio la ndege zisizo na rubani
Watu watatu wameripotiwa kuawaua Odesa Ukraine katika shambulio la ndege zisizo na rubani © FMM
Matangazo ya kibiashara

"Usiku, adui alishambulia Mkoa wa Odesa na ndege zisizo na rubani," viongozi wa mkoa walisema katika taarifa kwenye mtandao wa kijamii, wakimaanisha vikosi vya Urusi.

Vikosi vya ulinzi wa anga vya Ukraine viliharibu ndege zote zisizokuwa na rubani lakini vifusi vyake vilivyoanguka viligonga jengo la makazi ya juu, na kusababisha moto, ilisema taarifa hiyo.

"Kwa bahati mbaya, kuna wahasiriwa miongoni mwa raia," maafisa walisema, na kuongeza kuwa watu watatu waliuawa na wengine 26 wakiwemo watoto watatu kujeruhiwa.

Kando na hayo kamandi ya kusini mwa Ukraine ilisema moto huo ulizimwa lakini wimbi la mlipuko huo liliharibu majengo kadhaa ya ghorofa karibu.

Haya yanajiri wakati huu pia waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau akiwa mjini Kyiv kwa kile kimetajwa kuwa njia moja ya kuonyesha mshikamano na Ukraine wakati huu inapoendelea kushambuliwa na Urusi.

Trudeau pia ametembelea eneo la ukumbusho katikati mwa mji wa Kyiv ambako wanajeshi wa Ukraine ambao wameuawa na wapiganaji wanaoegemea upande wa Urusi wamezikwa tangu mwaka wa 2014.

Canada mwanachama wa NATO , imekuwa ikitoa msaada wa kijeshi na fedha kwa Ukraine tangu uvamizi wa Urusi mwezi Februari mwaka wa 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.