Pata taarifa kuu

Narendra Modi wa India amekutana na rais Zelensky pembeni ya mkutano wa G7

NAIROBI – Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alikutana na waziri mkuu wa India Narendra Modi moja kwa moja  kwa mara ya kwanza tangu nchi yake kuvamiwa na Urusi, uvamizi ambao New Delhi imekataa kuukashifu.

Waziri mkuu wa India amekuwa na makutano na rais wa Ukraine pembeni ya mkutano wa G7 nchini Japan
Waziri mkuu wa India amekuwa na makutano na rais wa Ukraine pembeni ya mkutano wa G7 nchini Japan © Narendra Modi
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao walikutana mjini Hiroshima, pembeni  ya mkutano wa wakuu wa nchi za G7, ambapo rais Zelensky aliwasili mapema leo Jumamosi kuhudhuria.

Hatua ya rais Zelensky kuhudhuria mkutano huo nchini Japan ikija baada ya  nchi ya Marekani kuahidi kuipa Kyiv ndege za kivita, ikiwa ni sehemu ya kile ambacho Kyiv imekuwa ikiomba kupewa.

Volodymyr Zelensky wa Ukraine baada ya kuwasili nchini Japan, amefanya mazungumzo na baadhi ya wakuu wa nchi za G7 wanaokutana nchini humo
Volodymyr Zelensky wa Ukraine baada ya kuwasili nchini Japan, amefanya mazungumzo na baadhi ya wakuu wa nchi za G7 wanaokutana nchini humo AFP - YUICHI YAMAZAKI

Zelensky pia amejadili kuhusu masuala yanahusiana na demokrasia na viongozi kutoka nchi saba kuu zilizoendelea za demokrasia zinazounda G7, pamoja na mataifa yaliyoalikwa yanayoendelea, ikiwa ni pamoja na India wanakutana.

Kupitia Ukurasa wake wa twitter, waziri mkuu Modi, amechapisha picha iliomuonyesha akisalmiana na Zelensky, ambapo pia wamefanya mazungumzo na maofisa wengine kutoka nchi hizo mbili.

Awali mkuu huyo wa Ukraine alikuwa amefanya mazungumzo na waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni na waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ambaye walikutana pia mapema mwezi huu wakati rais Zelensky alipokuwa akizuru bara Ulaya.

Kupitia Ukurasa wake wa twitter Zelensky alimshukuru waziri mkuu Sunak kwa kuipa nchi yake ndege za kijeshi.

 

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, akizungumza baada ya kukutana na rais Zelensky pembeni mwa kikao hicho ,amesema kuwepo kwa kiongozi huyo ilikuwa ni njia mwafaka zaidi wa kuelezea hali halisi Ukraine na kuyavutia mataifa zaidi kama Brazil na India kumuunga mkono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.