Pata taarifa kuu
UKRAINE- URUSI -NATO

Canada kununua silaha za ulinzi wa anga kutoka Marekani

Waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau, amesema serikali yake itanunua silaha za ulinzi wa anga kutoka Marekani na kuzitoa kwa Ukraine, lengo ni kuwapa uwezo wanajeshi wa Kiev kujilinda dhidi ya mashambulio ya Urusi.

 Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Canada
Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Canada REUTERS - PATRICK DOYLE
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa ulinzi wa Canada, Anita Anand, amesema silaha hizo zitagharimu zaidi ya dola milioni 406, kauli iliyoungwa mkono na Jumuiya ya NATO kupitia kwa katibu mkuu wake Jens Stoltenberg.

“Utawala wa Moscow unataka ulaya tofauti, unataka kudhibiti jirani zake na kuchukua demokrasia yake na uhuru” ameeleza Jens Stoltenberg.

Haya yanajiri wakati kuu NATO na umoja wa ulaya zikiahidi kuendelea kuisaidia Ukraine kujilinda dhidi ya mashambulio ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.