Pata taarifa kuu

Rushwa katika Bunge la Ulaya: Wanne wafungwa, ikiwa ni pamoja na naibu spika Eva Kaili

Katika faili ya kesi ya madai ya rushwa katika Bunge la Ulaya, watu wanne wameshtakiwa na kufungwa Jumapili hii, Desemba 11, ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Ubelgiji imebaini.

Kulingana na chanzo cha mahakama, Naibu spika wa Bunge la Ulaya Eva Kaili, raia wa Ugiriki (picha yetu) ni mmoja wa wale walioshtakiwa na kufungwa.
Kulingana na chanzo cha mahakama, Naibu spika wa Bunge la Ulaya Eva Kaili, raia wa Ugiriki (picha yetu) ni mmoja wa wale walioshtakiwa na kufungwa. AFP - ERIC VIDAL
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na chanzo cha mahakama, naibu spika wa Bunge la Ulaya Eva Kaili, raia wa Ugirki ni sehemu ya kundi hili. Polisi imefanya upekuzi pia katika nyumba ya mbunge wa pili wa Bunge la Ulaya, mamlaka nchini Ubelgiji imeongeza.

Watu wanne wanazuiliwa jela baada ya kushtakiwa na jaji wa Brussels kwa "kuhusishwa na kundi la uhalifu, utakatishaji wa pesa na ufisadi", umebaini upande wa mashtaka katika taarifa kwa vyombo vya habari, Jumapili hii, Desemba 11. Watu wengine wawili wameachiliwa na jaji.

Ofisi ya mwendesha mashitaka wa serikali haikutangaza majina ya watu hao wakati ilipotangaza saa sita mchana kuzuiliwa kwao kwa muda, uamuzi uliochukuliwa baada ya mashtaka manne ya "kuhusishwa na kundi la uhalifu, utakatishaji fedha na rushwa". Kwa mujibu wa chanzo cha mahakama kilicho karibu na kesi hiyo, kinachozungumza kwa sharti la kutotajwa jina, Eva Kaili ni mmoja wa watu hao wanne waliofungwa.

Hakuna kinga

Hakuweza kufaika na kinga yake ya ubunge kwa sababu kosa ambalo anashutumiwa lililonekana kuwa ni "kosa kubwa" siku ya Ijumaa, kimeeleza chanzo hicho. Chanzo hiki kimethibitisha ripoti za vyombo vya habari kwamba Bi Kaili alikuwa na "mifuko iliyojaa fedha" Ijumaa jioni wakati maafisa wa polisi wa Ubelgiji walipomkamata. Ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali pia imetangaza kuwa upekuzi ulifanyika Jumamosi jioni katika nyumba ya mbunge wa pili. Nyumba ya Bi Kaili inayopatikana mjini Brussels ilipekuliwa Ijumaa jioni.

Miongoni mwa washukiwa sita waliokamatwa siku ya Ijumaa, baada ya angalau misako 16 huko Brussels, pia ni wabunge wa zamani wa Italia Pier-Antonio Panzeri na katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi wa Kimataifa (ITUC) Luca Visentini, pia raia wa Italia. Kulingana na vyombo vya habari vya Ubelgiji, babake Bi Kaili mwenyewe alikuwa na wasiwasi katika uchunguzi huo, alinaswa akiwa na pesa "kwenye begi".

"Zawadi muhimu"

Taarifa ya mwendesha mashtaka wa umma inasisitiza kwamba katika kesi hii 'malipo ya kiasi kikubwa cha pesa au utoaji wa zawadi muhimu kwa watu wa tatu wenye msimamo wa kisiasa na / au wa kimkakati utaowezesha, ndani ya Bunge la Ulaya, kushawishi maamuzi' ya taasisi hii. Haya yote kwa manufaa ya nchi ya Ghuba, iliyotambuliwa kwenye vyombo vya habari kama Qatar.

Jumamosi jioni, Spika wa Bunge la Ulaya, Roberta Metsola wa Malta, aliamua juu ya vikwazo vya kwanza dhidi ya Eva Kaili. Naibu Naibu spika wa Bunge la Ulaya alipokonywa majukumu yote aliyokabidhiwa na Bi Metsola, likiwemo la kumwakilisha katika eneo la Mashariki ya Kati. Wabunge wa mrengo wa kushoto, akiwemo mwanaikolojia Philippe Lamberts kwa niaba ya kundi la Greens katika Bunge la Ulaya, walimtaka Bi Kaili kujiuzulu, ambaye alifutwa katika Chama cha Kisoshalisti cha Ugiriki (Pasok-Kinal) Ijumaa jioni.

Huko Brussels, uchunguzi unaendelea, upekuzi mpya ulifanyika nyumbani kwa mbunge mwingine. Kwa mujibu wa magazeti ya Le Soir na Knack, ni mwanasoshalisti aliyechaguliwa wa Ubelgiji Marc Tarabella. 

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.