Pata taarifa kuu

Spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi kuzuru Taiwan Beijing ikionya

China imeionya Marekani kuhusu mpango wa spika wa bunge nchini humo Nancy Pelosi wa kutaka kuzuru Taiwan. Iwapo ziara hii itafanikishwa, kiongozi huyo atakuwa mtu wa ngazi ya juu katika serikali ya Washington kuzuru kisiwa hicho tangu mwaka 1997.

Spika wa bunge la Marekani- Nancy Pelosi
Spika wa bunge la Marekani- Nancy Pelosi REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Washington imeonekana kuighadhabisha China ambayo na yenyewe umeonyesha nia ya kutaka Taiwan inayojitawala kuwa sehemu yake.

Utawala wa Biden umeripotiwa kumshawishi Pelosi kuwazia tena nia ya kufanya zaira nchini Taiwan.

Juma lilopita rais Joe Biden katika taarifa yake kwa wanahabari alitaja kuwa jeshi limeonelewa kuwa ziara hiyo haikuwa wazo bora. White House na yenyewe ikieleza kuwa ziara hiyo sio ya lazima na haitasaidia lolote.

Nayo wizara ya mambo ya kigeni imeeleza kwamba Pelosi hajatangaza mpango wowote wa kusafiri na msimamo wa Marekani kuhusu Taiwan haujabadilika.

Marekani imeendelea kusisitiza msimamo wake kuwa uhusiano wake na Taiwan sio rasimi Washington ikisema kwamba ina uhusiano rasimi na china na wala sio Taiwan.

Iwapo ziara ya Pelosi itatokea, itakuja wakati huu ambapo wasiwasi kati ya Washington na Beijing ukionekana kupanda kuelekea mazungumzo ya njia ya simu yanayotarajiwa kufanyika kati ya Joe Biden wa Marekani na kiongozi wa China Xi Jinping.

Baadhi ya raia wa Marekani na viongozi wa Congress wameonekana kugawanyika kuhusu ushirikiano na Taiwan.

Spika wa bunge Nancy Pelosi ameonekana kuwa mkosoaji mkubwa wa china. Akiituhumu kwa kuhusika na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.

Pelosi alitarajiwa kuzuru Taiwan mwezi Aprili japokuwa ziara yake iliairishwa baada yake kuambukizwa uviko 19.

Kiongozi huyo amekataa kuzungumzia sababu ya ziara yake japokuwa wiki jana alinukuliwa akisema kuwa kuna umuhimu wa kuonyesha uungwaji mkjono kwa Taiwan. Beijing inaiona Taiwan kama moja ya sehemu yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.