Pata taarifa kuu
NEW ZEALAND- AFYA.

New Zealand: Serikali kutoa barakoa bila malipo kwa raia kukabiliana na Uviko-19

Serikali ya New Zealand imesema itatoa barakoa na vifaa vingine vya kupima Uviko 19 kwa raia wakati huu taifa hilo likiwa mbioni kudhibiti maambukizi mapya ya ugonjwa huo pamoja na kabiliana na mlipuko wa homa inayosemekana kuwatatiza raia nchini humo.

Chanjo ya uviko 19.
Chanjo ya uviko 19. AFP - JUSTIN TALLIS
Matangazo ya kibiashara

Takriban watu elfu 70 wamethibitishwa kuambukizwa Uviko 19, wagonjwa 765 wakiwa wamelazwa baada ya kuambukizwa.

New Zealand yenye idadi ya watu zaidi ya milioni tano imesajili zaidi ya visa elfu kumi na moja vya uviko 19 kwa siku moja peke.

Maofisa wa afya nchini humo aidha wanatoa wito kwa raia kujitokeza kwa wingi kuchoma chanjo ya pili kuwakinga na kasi ya maambukizi hayo.

Taarifa ya serikali imeeleza kuwa uvaaji wa barakoa unaweza punguza uwezo wa kuambukizwa uviko 19 kwa asilimia 53.

New Zealand ilikuwa mojawapo ya mataifa yaliotanagaza sheria kali za kabiliana na uviko 19 katika kipindi cha miaka sita iliyopita kabla ya kulegeza sheria hizo kutokana na kasi ndogo ya maambukizi baada ya idadi kubwa ya raia kuchoma chanjo.

Taifa hilo liliaanza kufungua baadhi ya  mipaka yake  na mataifa mengine mapema mwaka huu na inatarajiwa kufungua kikamilifu ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.