Pata taarifa kuu
MAREKANI- UCHUMI

Marekani, Japan zakubaliana kushirikiana kiuchumi kufuatia mzozo wa Ukraine.

Maofisa wa ngazi ya juu  katika sekta ya uchumi kutoka kwa serikali  ya Marekani na Japan katika mkutano wao jijini Tokyo, wamefiakia kufanya kazi kwa pamoja ilikabiliana na mfumuko wa bei za chakula na gesi ambapo wameendelea kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Janet Yellen, Waziri wa fedha wa Marekani.
Janet Yellen, Waziri wa fedha wa Marekani. © Leah Millis/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen na mwenzake wa Japan Shunichi Suzuki wameeleza kuwa vita kati ya Urusi na Ukraine ni tishio kwa uchumi.

Japan na Marekani aidha zimeahidi kuleta nguvu pamoja kutatua changamoto za kifedha chini ya uanachama wa G7 na G20.

Viongozi hao wameahidi kushirikiana ilikuisaidia Kyiv kabiliana na chanagomoto za kiuchumi zinazoikabili wakikashifu hatua ya Moscow kiushambulia Kyiv.

Japan, inategemea pakubwa uwagizaji wa mafuta kutoka mataifa mengine ambapo imekuwa ikipitia wakati mgumu kupata bidhaa hiyo kutokana na vita dhidi ya Urusi na Ukraine.

Yellen, anatarajiwa kufanya ziara nchini Indonesia siku ya jumatano ambapo atakutana na Suzuki na maofisa wa fedha kutoka katika mataifa ya G20.

Kikao cha maofisa hao kinatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 12-16 mwezi Julai kabla ya Yellen kusafiri kuelekea Korea kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.