Macron asema Urusi haipaswi kushinda vita dhidi ya Ukraine
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameisthumu Urusi kwa kujaribu kukwamisha utaratibu wa Kimataifa kwa kukwamisha kusambaa kwa chakula duniani, na kusema kuwa nchi hiyo haipaswi kushinda vita vinavyoendelea.
Imechapishwa:
Cheza - 00:31
“Urusi haipaswi kushinda vita hivi, na vikwazo vitasalia kwa muda mrefu,” amesema.
Akizungumza wakati wa kuufunga mkutano wa G 7 nchini Ujerumani, ambako viongozi wa nchi hizo wameahidi kutoa Dola Bilioni 5 kusaidia kusuluhisha uhaba na kupanda bei ya chakula duniani.
“Ufaransa nayo itatoa msaada wa Euro 700,000 kuhakikisha kuna usalama wa chakula,” ameongeza.
Usalama umeimarishwa kwenye mkutano huo ambao kwa kisiasa kikubwa utazungumzia vita vya Ukraine na Urusi.