Pata taarifa kuu

New Zealand kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa Ukraine

Serikali ya New Zealand imetangaza kwamba itatuma nchini Uingereza takriban wakufunzi thelathini wa kijeshi kuwafunza wapiganaji wa Ukraine katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Mwanajeshi akiwa katika ulinzi karibu na uwanja wa vita huko Brovary, nje kidogo ya Kyiv, Ukraine, Jumatatu, Machi 28, 2022.
Mwanajeshi akiwa katika ulinzi karibu na uwanja wa vita huko Brovary, nje kidogo ya Kyiv, Ukraine, Jumatatu, Machi 28, 2022. AP - Rodrigo Abd
Matangazo ya kibiashara

Wakufunzi hawa wa New Zealand watatoa mafunzo kwa askari wa Ukraine kutumia bunduki ndogo za kivita za 105mm L119. Takriban  wapiganaji 230 watanufaika na mafunzo haya, yatakayodumu hadi mwisho wa mwezi wa Julai.

New Zealand tayari imetuma ndege ya Hercules na wanajeshi kwenda Ulaya kwa shughuli za usafirishaji na ujasusi kusaidia Ukraine kujihami dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Wakati huo huo Ukraine imeirefusha hali ya dharura ya sheria ya kijeshi kwa miezi mitatu zaidi hadi Agosti 23 huku vita vyake na Urusi vikiendelea. Rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelensky alitia saini kwa mara ya kwanza amri hiyo mnamo Februari 24 wakati walipovamiwa na vikosi vya Urusi.

Bunge la Ukraine limepiga kura kwa wingi kupitisha muswada huo unaoongezwa kwa mara ya tatu katika kipindi ambacho Urusi ikiendeleza mashambulizi yake na kulilenga eneo la mashariki la Donbas.

Baada ya kushindwa kuudhibiti mji mkuu wa Kyiv, Moscow ilielekeza tangu mwezi Machi harakati zake mashariki mwa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.