Pata taarifa kuu

Ukraine: Mikutano mitatu ya kilele ya kidiplomasia imepangwa kufanyika Alhamisi

Siku ya 29 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Alhamisi Machi 24, mikutano mitatu ya kilele (G7, NATO, EU) imepangwa kufanyika huko Brussels, nchini Ubelgiji. Nchi za Magharibi zinakusudia kuimarisha hatua dhidi ya Urusi ili kuendelea kwa muda mrefu.

Rais Joe Biden anaondoka kwenye Marine One na kuingia kwenye Air Force One kwenye Kwenye kambi ya jeshi la wanaanga ya Andrews, Maryland, Jumatano, Machi 23, 2022. Aliwasili Brussels saa chache zilizopita.
Rais Joe Biden anaondoka kwenye Marine One na kuingia kwenye Air Force One kwenye Kwenye kambi ya jeshi la wanaanga ya Andrews, Maryland, Jumatano, Machi 23, 2022. Aliwasili Brussels saa chache zilizopita. AP - Gemunu Amarasinghe
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Urusi bado vinauzingira mji mkuu wa bandari ya kusini, Mariupol. Majeshi ya Ukraine yamejibu mashambulizi ya majeshi ya Urusi na kufaulu kurejesha kwenye himaya yake eneo moja karibu na mji mkuu wa Kyiv.

 

Pointi kuu:

► Alhamisi hii, nchi za Magharibi zinakutana mjini Brussels kwa mikutano mitatu: ule wa NATO asubuhi ya leo na ule wa G7 na Baraza la Ulaya mchana. Joe Biden aliwasili katika mji mkuu wa Ubelgiji usiku wa leo kushiriki katika mikutano hiyo. Kisha atasafiri kwenda Poland.

► Wanajeshi wa Urusi bado wanajaribu, bila mafanikio, kuziKngira mji wa Kyiv. Baadhi ya maeneo ya makazi ya mji mkuu yalilengwa na mashambulizi ya anga siku ya Jumatano. Mashambulio ya anga yanaendelea katika miji mingi ya Ukraine, kama vile Kharkiv, Mariupol, Odessa, Mykolaiv, lakini bila maendeleo makubwa ya kimkakati.

► Kyiv na Moscow kila upande moja umeelezea kuwa mazungummzo na Urusi kuwa "magumu" , mazungumzo yaliyofanyika kwa nia ya kusitisha uhasama, pande hizo mbili zikikataa kuwajibika kwa vizuizi. Baada ya duru kadhaa za mazungumzo ya ana kwa ana, na ambayo yanaendelea mtandaoni, amesema kiongozi wa ujumbne wa Ukraine katika mazungumzo.

► Rais wa Ukraine alizungumza kwa njia ya video na wabunge wa Ufaransa Jumatano hii, Machi 23 ili kupata uungwaji mkono zaidi kutoka kwa Ufaransa katika kukabiliana na vita vinavyoendeshwa na Urusi. Mapema siku ya Jumatano, alihutubia bunge la Japan, akitaka mageuzi ya Umoja wa Mataifa.

► Volodymyr Zelensky alisema katika video iliyotolewa Jumanne jioni kwamba watu 100,000 wanaishi katika Mariupol iliyozingirwa katika "hali isiyo ya kibinadamu". Mamlaka imetangaza juhudi mpya za kujaribu kuwahamisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.