Pata taarifa kuu

Georgia yafanya uchaguzi baada ya kukamatwa kwa Mikheil Saakashvili

Katika Caucasus, Wajiorgia wanachagua wajumbe wa serikali za mitaa Jumamosi hii, Oktoba 2. Ni uchaguzi unaochukuliwa kuwa muhimu kwani unakuja wakati hufo ikitanda katika jamhuri hii ya zamani ya Soviet.

Jumamosi hii, Oktoba 2, Wajiorgia wamewachagua mameya na madiwani. Uchaguzi umeonekana kuwa muhimu kwani unakuja katika muafaka.
Jumamosi hii, Oktoba 2, Wajiorgia wamewachagua mameya na madiwani. Uchaguzi umeonekana kuwa muhimu kwani unakuja katika muafaka. REUTERS - IRAKLI GEDENIDZE
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hili limefanyika Jumamosi hii Alaasiri kwa amani na kwa utaratibu mzuri . Kufikia saa 6 mchana (saa za Gerogia), 18% kati ya wapiga kura milioni tatu na nusu wa Georgia walikuwa wametimiza wajibu wao wa kiraia.

Uchaguzi huu ni muhimu kwa sababu ya mvutano kati ya chama tawala, "Ndoto ya Georgia" cha Bidzina Ivanishvili, na wapinzani wake. Ijumaa Oktoba 1, Mikheïl Saakachvili, rais wa Georgia kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2013, alikamatwa baada ya kurejea nchini kwa siri, baada ya miaka minane akiwa uhamishoni.

Uchaguzi katikati ya mgogoro wa kisiasa

Lakini kukamatwa kwa rais wa zamani Mikhail Saakashvili ni wazi hakukuvuruga nia ya kupiga kura ya Wajiorgia. Wapiga kura hata hivyo walichanganyikiwa, baada ya kampeni ambapo vikosi vilivyokuwepo vilizungumza kidogo sana juu ya "mpango" huo na walitumia muda mwingi kukosoana.

Maisha ya kisiasa ya Georgia yamekumbwa na mizozo ambayo imechochewa kwa karibu miaka mitatu. Chama tawala cha "Ndoto ya Wajiojia" kinalaumu wapinzani wake kwa msimamo mkali, kuanzia kwa chama cha Umoja wa Kitaifa ya Mikheil Saakashvili.

Vyama vingi vya upinzani yanalaani kutekwa kwa taasisi za serikali na chama tawala na kiongozi wake, Bidzina Ivanishvili, ambaye pia anatuhumiwa kuiga Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.