Pata taarifa kuu
NEW-ZEALAND-MAUAJI-USALAMA

New Zealand: Arobaini wauawa katika mashambulizi dhidi ya miskiti miwili Christchurch

Watu 40 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya baada ya watu wane kufanya mashambulizi katika msikiti miwili katika mji wa Christchurch, Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amesema.

Kikosi maalum cha AOC (Armed Offenders Squad) vinafanya operesheni ya kuwasaka wahalifu walioendesha mashambulizi dhidi ya misikiti miwili huko Christchurch, New Zealand, Machi 15, 2019.
Kikosi maalum cha AOC (Armed Offenders Squad) vinafanya operesheni ya kuwasaka wahalifu walioendesha mashambulizi dhidi ya misikiti miwili huko Christchurch, New Zealand, Machi 15, 2019. REUTERS/SNPA/Martin Hunte
Matangazo ya kibiashara

Maofisa wa polisi wametumwa katikati mwa jiji la Christchurch baada ya mashambulizi ya risasi katika misikiti miwili nchini New Zealand. Polisi, ambayo inasema "watu wengi wameuawa, imewakamata watu kadhaa.

Kwa mujibu wa chanzo cha polisi katika eneo la tukio, vizuizi vimeanza kuondolewa kwenye barabara za mji huo mara baada ya polisi kutangaza kuwa wamekamata watu wanne na mabomu yaliyotengenezwa kienyeji.

"Watu wane, wanamume watatu na mwanamke mmoja, wanashikiliwa na polisi, " amesema, mkuu wa polisi katika eneo hilo Mike Bush, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, huku akibiani kwamba jeshi lilitegua kilipuzi kilichopatikana katika magari ya watuhumiwa.

Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia.

Amemtaja mshukiwa wa shambulio hilo kuwa "gaidi mwenye itikadi kali za mrengo wa kulia".

Awali mkuu wa pilisi katika mji wa Christchurch amesema watu waliouawa ni wengi, lakini hakutaja idadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.