Pata taarifa kuu
CETA-EU-CANADA

Hatimaye EU na Canada zatiliana saini mkataba wa kibiashara wa CETA

Waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau na viongozi wa umoja wa Ulaya, hatimaye wametiliana mkataba wa kibiashara wa kihistoria baina ya pande hizo mbili, baada ya miaka kadhaa ya majadiliano na kuchelewesha kwa shughuli hiyo juma moja lililopita na viongozi wa Wallonia nchini Ubelgiji.

Waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau (katikati) akiwa na rais wa umoja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker (kushoto wa kwanza) pamoja na mkuu wa tume ya Ulaya, Donald Tusk, October 30, 2016
Waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau (katikati) akiwa na rais wa umoja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker (kushoto wa kwanza) pamoja na mkuu wa tume ya Ulaya, Donald Tusk, October 30, 2016 REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Sherehe za utiaji saini jijini Brussels, zilicheleweshwa kutoka Alhamisi ya juma lililopita, baada ya wakuu wa eneo la Wallonia nchini Ubelgiji, lenye wakazi milioni 3 pekee, kupiga kura kuzuia kutiwa saini kwa mkataba huo, wakitaka kwanza hakikisho la mkataba ambao sasa utakuwa na athari chanya kwa watu zaidi ya milioni 500 parani Ulaya na watu milioni 35 nchini Canada.

Shangwe na makofi yalishuhudiwa wakati ambapo waziri mkuu Trudeau alipokuwa akitia saini mkataba huu sambamba na rais wa umoja wa Ulaya Donald Tusk, mkuu wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker na waziri mkuu wa Slovakia Robert Fico, ambaye nchi yake inashikilia urais wa umoja wa Ulaya kwa sasa.

Awali kabla ya sherehe hizo, waandamanaji walifanikiwa kuvuka vizuizi vya polisi na kufika nje ya jengo la makao makuu ya umoja wa Ulaya na kuchora vioo vya jengo hilo, wakikashifu makubaliano haya ya kibiashara ya "Comprehensive Economic and Trade Agreement' maarufu kama CETA.

Rais wa EU, Juncker(kushoto), waziri mkuu wa Canada, Trudeau (anayefuatia kutoka kushoto), mkuu wa tume ya EU, Tusk na waziri mkuu wa Slovakia, Robert Fico, October 30, 2016.
Rais wa EU, Juncker(kushoto), waziri mkuu wa Canada, Trudeau (anayefuatia kutoka kushoto), mkuu wa tume ya EU, Tusk na waziri mkuu wa Slovakia, Robert Fico, October 30, 2016. REUTERS/Francois Lenoir

"Safi sana, safi sana," alisikika akisema waziri mkuu Trudeau wakati alipokuwa akimkumbatia rais wa Ulaya Tusk na mkuu wa tume hiyo Juncker, alipokuwa akiwasili kwenye eneo la tukio lililokuwa na ulinzi mkali.

"Subira yavuta heru," alijibu Juncker na kuongeza kuwa huu ni wakati muhimu sana kwa umoja wa Ulaya na Canada kwasababu tunatengeneza viwango vya kimataifa ambavyo vitafuatwa na watu wengine pia'. alimaliza.

Kuanza kwa sherehe za utiaji saini pia zilicheleweshwa zaidi hii leo, wakati ndege ya waziri mkuu Trudeau ilipolazimika kurejea ilipotoka kutokana na hitilafu za kiufundi.

Mkataba huu wa CETA unaondoa vikwazo vya tozo za kibiashara kwa zaidi ya asilimia 99 kati ya nchi hizo mbili, ukiuunganisha umoja wa Ulaya na taifa ambalo ni la 10 kidunia kwa kuwa na uchumi imara duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.