Pata taarifa kuu
UJRUMANI-SIASA-JAMII

Ujerumani: Kansela Helmut Schmidt afariki akiwa na umri wa miaka 96

Helmut Schmidt, kiongozi wa zamani wa kutoka chama cha Social Democrat ambaye alikuwa Kansela wa Ujerumani katika miaka ya 1974-1982 amefariki leo Jumanne, Novemba 10, wakati ambapo afya yake ilikuwa mbaya mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Schmidt, Januari 19, 2014.
Kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Schmidt, Januari 19, 2014. REUTERS/Fabian Bimmer/Files
Matangazo ya kibiashara

Alilazwa hospitalini mwezi Agosti kwa upungufu wa maji mwilini na kufanyiwa upasuaji mwezi Septemba kwa tone la damu katika mguu, Helmut Schmidt, tangu wakati huo, alirudi nyumbani katika mji wa Hamburg (kaskazini).

Kwanza ni kumbukumbu ya mgogoro ambao anaacha Kansela Helmut Schmidt hata kabla ya kuingia madarakani mwaka 1974. Wakati alipomrudilia kiongozi mwingine kutoka chama cha Social-Democrat, Willy Brandt, Helmut Schmidt alikuwa tayari kuongea naye dhidi ya mafuriko katika mji wa Hamburg, mji alikozaliwa mapema katika miaka ya 1960 au kwa kupambana na wanafunzi wa mrengo wa kushoto, katika muongo mmoja.

Katika uongozi wake, kwa kipindi cha miaka miaka nane, pia kulishuhudiwa migogoro mikubwa. Bila shaka mgogoro wa kwanza wa kiuchumi, mgogoro wa kwanza wa mafuta, lakini pia mgogoro wa ndani pamoja na kuanzishwa kwa uasi wa Red Army, kundi la kigaidi la mrengo wa kushoto ambalo lilimlazimisha kuchukua hatua ngumu na pia dhidi ya kambi ya chama cha Social-Democrata kwa kulazimisha kupelekwa kwa makombora ya Marekani Ujerumani ya Magharibi dhidi ya jeshi la Urusi ya zamani (SS20).

Wakati wa uongozi wake, Helmut Schmidt kwanza aliheshimiwa zaidi kuliko kupendwa. Tangu alipokua mpenzi wa Wajerumani kufuatia vitabu thelathini, ambapo vingi miongoni mwa vitabu hivyo viliuzwa kwa kiasi kibwa na uwepo muhimu katika mjadala wa umma, na aliongoza kwa kipindi kirefu gazeti maarufu la kila wiki la die Zeit, pia alikua akiandika mahali pengine, lakini mara nyingi alionekana katika vyombo vya habari, alikuwa bila shaka mwanasiasa aliye pendwa sana na Wajerumani Wajerumani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.