Pata taarifa kuu
GEORGIA

Mbunge zamani nchini Georgia atiwa nguvuni kwa tuhuma uhaini

Polisi nchini Georgia wamemkamata aliyekuwa mbunge wa zamani wa nchi hiyo Valery Gelbakhian kwa tuhuma za kuhusika na njama za kutaka kuipindua serikali mwaka 2008.

Wakili wa mbunge zamani nchini Georgia Valery Gelbakhian
Wakili wa mbunge zamani nchini Georgia Valery Gelbakhian
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi nchini humo imesema kuwa Gelbakhiani alikamatwa mpakani mwa nchi hiyo na Armenia ambapo alikuwa akijaribu kutoroka baada ya kutolewa kwa taarifa za kukamatwa kwake.

Gelbakhiani ambaye alikuwa mshirika mkuu wa kiongozi wa upinzani na tajiri Badri Patarkatsishvil anatuhumiwa kupanga njama za kutaka kuipindua serikali ya rais Mikheil Saakashvili mwaka 2008.

mbunge huyo alirekodiwa kwenye mkanda wa video unaomuonesha kushiriki mazungumzo ya kutaka kuipindua serikali ya Mikheil Saakashvil.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.