Pata taarifa kuu

Gaza: Wajumbe wa Hamas na Israel waondoka Cairo, juhudi za upatanishi 'zinaendelea'

Wawakilishi wa Hamas kutoka Palestina na Israel wameondoka Cairo "baada ya siku mbili za mazungumzo" yenye lengo la kupata suluhu katika vita vinavyoendelea Gaza kwa muda wa miezi saba, Al-Qahera News, shirika la habari lililo karibu na idara ya ujasusi nchini Misri, limeripoti siku ya Alhamisi.

Uharibifu unaofanywa na Israel huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Mei 9, 2024.
Uharibifu unaofanywa na Israel huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Mei 9, 2024. REUTERS - Hatem Khaled
Matangazo ya kibiashara

Juhudi za Misri na nchi nyingine za upatanishi, ambazo ni Qatar na Marekani, "zinaendelea kuleta maoni ya pande hizo mbili karibu zaidi," Al-Qahera News iliongeza, ikitoa mfano wa chanzo cha Misri kutoka ngazi ya juu.

Ofisi ya Hamas mjini Beirut, mji mkuu wa Lebanon, imethibitisha kuondoka kwa ujumbe wa kundi hilo lililo madarakani katika Ukanda wa Gaza. Kutoka Cairo, wajumbe wanaelekea Doha nchini Qatar.

Israel na Hamas hazijadili moja kwa moja. Misri, Qatar na Marekani zinapatanisha mzozo huu ili kufanikisha kuachiliwa kwa mateka wa Israeli ambao bado wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza, kwa kubadilishana na kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina na usitishaji wa mapigano katika eneo hili la takriban kilomita 360 linaloendelea kushambuliwa na jeshi la Israel.

Kwa mujibu wa Ezzat al-Rishq, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, operesheni zinazofanywa na jeshi la Israel huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, "zinalenga kuzuia juhudi za wapatanishi". Katika taarifa yake, amebainsha kujitolea kwa Hamas "kukubali pendekezo lililowasilishwa na wapatanishi."

Maelfu ya Wapalestina waoishi kwenye mji wa Rafah wenye wakaazi zaidi ya Milioni 1.5, wameendelea kukimbilia maeneo mengine, wakati huu  jeshi la Israel likitekeleza mashambulio, licha ya pingamizi kutoka Jumuiya ya Kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.