Pata taarifa kuu

Hali ya wasiwasi yatanda katika mji wa Rafah, baada ya Israel kutekeleza mashambulizi

Jeshi la Israeli limeshambulia mji wa Rafah kwenye ukanda wa Gaza, baada ya kutuma magari ya kijeshi kabla ya kuanza operesheni ya ardhini, wakati huu mazungumzo ya kujaribu kutafuta mwafaka wa kusitisha vita na Hamas, yakirejelewa jijini Cairo.

Wapalestina wanatazama uharibifu baada ya mashambulizi ya Israeli huko Rafah, Mei 7, 2024.
Wapalestina wanatazama uharibifu baada ya mashambulizi ya Israeli huko Rafah, Mei 7, 2024. © AP/Ismael Abu Dayyah
Matangazo ya kibiashara

Licha ya shinikizo kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa kuitaka Israeli kutotuma wanajeshi wake wa ardhini kwenye mji wa Rafah, siku ya Jumanne ilituma magari yake ya kivita, karibu na mpaka wa Misri.

Hata hivyo, Israeli imesema imefungua vivukio viwili, vinavyoingia Gaza vya , Kerem Shalom na Erez ili kuruhusu misaada ya kibinadamu, hatua inayokuja baada ya shinikizo za Kimataifa.

Hata hivyo, Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, inasema kivukio cha Kerem Shalom bado hakijafunguliwa.

Katika hatua nyingine, shinikizo zinaendelea kutolewa kwa Israeli kutoendelea na mpango wake wa kutuma vikosi vya ardhini kwenye mji wa Rafah na Qatar, nchi mojawapo inayoongoza mazungumzo ya kupata mwagaka ikitoa wito kwa Jumuiya ya Kimataufa kuizuia Israel, kwa hofu ya kutokea kwa mauaji makubwa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ameendelea kusisitiza kuwa operesheni kwenye mji wa Rafah ni muhimu sana ili kuwazuia Hamas kuwa na kambi kwenye mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.