Pata taarifa kuu

Israeli imesikitishwa na matamshi ya Biden kuhusu msaada wa kijeshi

Balozi wa Israeli katika Umoja wa Mataifa Gilad Erdan ameeleza kusikitishwa na matamshi ya rais Joe Biden wa Marekani Jumatano ya wiki hii kuwa nchi yake  itasitisha msaada wa baadhi ya silaha kwa nchi  ya Israeli ikiwa taifa hilo litashambulia mji wa Rafah ulioko kusini mwa Gaza.

Joe Biden și Benjamin Netanyahu
Rais Joe Biden wiki hii alitishia kusitisha usambazaji wa baadhi ya silaha kwa Israeli iwapo itaishambulia Rafah. AP
Matangazo ya kibiashara

Kwa muda sasa mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na washirika wa Israel, wamekuwa wakishinikiza nchi hiyo kuachana na mpango wowote wa kushambulia mji wa Rafah, ambao ni makao kwa mamilioni ya raia waliokimbia kutoka Gaza.

Hii ikiwa ni kauli ya kwanza kali kutolewa na mshirika wa karibu wa utawala wa Tel-Aviv kutokana na oparesheni zake za kijeshi katika eneo la Rafah.

Soma piaIsraeli imetuma magari kivita kwenye eneo la Rafah katika ukanda wa Gaza

Zaidi ya raia wa Palestina milioni moja wamepewa hifadhi katika eneo hilo baada ya kutoroka mapigano katika maeneo mengine ya mji wa Gaza.

Biden, katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CNN, amesisitiza kuendelea kusimama na Israeli katika vita vya na kundi la Hamas lakini iwapo mshirika wake angeivamia Rafah basi nchi yake italazimika kusitisha mpango wa kuihami Israeli.

Kihistoria, Marekani imekuwa ikiipa Israeli msaada mkubwa wa kijeshi na iliongeza msaada huo baada ya shambulio la Hamas la tarehe 7 ya mwezi Oktoba katika ardhi ya Israeli.

Karibia raia 1,200 wa Israeli wakiwemo watoto na wanawake waliripotiwa kuuawa wakati wa shambulio hilo la Hamas, watu wengine 250 wakichukuliwa mateka.

Awali rais Biden alikuwa ametangaza kusitishwa kwa usafirishaji wa mabomu kwenda nchini Israeli kwa madai kuwa huenda wanajeshi wa Israeli wangeyatumia kutekeleza uvamizi katika eneo la Rafah.

Soma piaMashambulizi Rafah: Marekani yasitisha kuipa mabomu Israeli

Haya yanajiri wakati huu shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi wa Palestina likisema kwamba raia elfu 80 wa Palestina wametoroka katika eneo la Rafah katika kipindi cha siku tatu tangu Israeli kuongeza kasi ya mashambulio katika mji wa kusini mwa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.